Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na Mabalozi wastaafu kwa mujibu wa sheria.
Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:


1. Balozi Dora Mmari Msechu (kushoto); ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Stockholm, nchini  Sweden. Hadi uteuzi huu unafanyika Balozi Dora Mmari Msechu ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Anachukua nafasi ya Balozi Mohamed M .H. Mzale ambaye amestaafu.



2. Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba (kulia), ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Moscow, Urusi. Hadi uteuzi huu unafanyika, Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba alikuwa Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo, Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Anachukua nafasi ya Balozi Jaka Mwambi.



3. Kadhalika, Mheshimiwa Rais amemteua Ndugu Joseph Edward Sokoine  (kushoto) kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kabla ya uteuzi huu, Bw. Sokoine alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Ottawa, Canada.



               Umetolewa na:

(John M. Haule)
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NJE
NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana tena sana ndugu yetu Sokoine. In fact, this appointment is well overdue. If you knew Edward Moringe Sokoine, you will agree that Joseph is just like his father. You will be highly missed in Ottawa Sokoine. We are really praying that you become a minister in any powerful ministry in Tanzania. You deserve it...

    ReplyDelete
  2. Wow! He looks so much like his father. Edward Moringe Sokoine very few like him! I was in Primary school when Hon Sokoine died, but I knew it was something terribly big. In Arusha it was like the sun is suddenly lost and nowhere to be found. I am sure Tanzania would have been much better today if Sokoine was alive. He was the man not talk talk leader like the ones we have now, he was the man in action, a man of mission a corruption free leader. God bless you all

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...