Kwa niaba ya uongozi wa Jumuiya ya Wanataaluma
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) kwa kushirikiana na Idara ya Sayansi ya Siasa na
Utawala napenda kuwakaribisha kwenye
Kongamano la Muungano litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Nkrumah siku ya
Jumamosi tarehe 26 Aprili 2014.
Kongamano hilo litaanza saa 7.30 mchana hadi
saa 12 jioni ndani ya UKUMBI WA NKRUMAH
WA CHUO KIKUU CHA DARE ES SALAAM. Mada kuu ya Kongamano hilo ni, «Tujadili na Tutafakari Mustakabali wa Muungano wetu»
Kutakuwa na mada tatu za kujadiliwa na watoa
mada kwenye mabano:
1) Chanzo au Mchakato wa Kisiasa wa
kuwa na Muungano ( Prof. Mohammed Bakari)
2) Tathmini ya Miaka 50 ya Muungano
(Dkt Alexander Makulilo)
3) Mustakabali wa Muungano (Prof.
Gaudence Mpangala)
Tunaomba kwa yeyote mwenye maoni basi asisite
kututumia kwa barua pepe kwa anwani : kongamanoudasa@gmail.com.
Asanteni sana
Bw. Faraja Kristomus
(Katibu – UDASA)
0787 52 53 96 / 0717 086 135
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...