Mhe. Sophia
M. Simba (Mb) na Familia yake, anatoa
shukrani zake za dhati kwa wote walioshirikiana naye katika kipindi kigumu cha
kumuuguza mtoto wake mpendwa LEEFORD C.
CENGE SIMBA (pichani), hadi alipoiaga dunia tarehe 06 Machi, 2014 katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili na kuzikwa tarehe 08 Machi, 2014 katika makaburi ya
Kinondoni.
Kwa heshima kubwa tunatoa shukrani za dhati
kwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Mohamed Gharib Bilal Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Marais wastaafu ,Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe.
Ali H. Mwinyi, Mhe, Mizengo K. P. Pinda
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, IGP Ernest Mangu , Mhe. Meck Sadick Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Uongozi na
Wafanya kazi wote wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Wahe.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, majirani, ndugu, marafiki wa Masaki,
Magomeni, Ilala Upanga, na sehemu
mbalimbali za Dar es salaam na Tanzania
kwa ujumla, na wale wote wenye mapenzi
mema kwa sala na dua zao katika kipindi hiki kigumu.
Shukrani za pekee ziwaendee Madaktari na
wafanya kazi wote wa Hospitali ya Shri HinduMandal chini ya uongozi wa Daktari
Kaushik akishirikiana na Madaktari mahiri, Dr Amar na Dr Mwanaada, na vilevile
sista Mapunda kwa upendo na huduma nzuri
aliyoitoa.
Kwa vile si rahisi kumshukuru kila mmoja,
tunaomba mkubali shukrani zetu za dhati kwa kushirikiana nasi katika mazishi ya
kijana wetu.
Aidha tunaushukuru uongozi wa kanisa katoliki
la Mashahidi wa Uganda Magomeni na
kanisa la Mtakatifu Petro la Oysterbay
kwa kuendesha Ibada ya mazishi.
Tunawakaribisha kujumuika nasi katika Ibada ya Misa Takatifu
ya kumuombea Marehemu, itakayofanyika katika kanisa Katoliki la Mashahidi wa
Uganda - Magomeni, Dar es salaam tarehe
27 Aprili, 2014 saa 02.30 asubuhi.
Tutahitimisha kwa chakula cha mchana,
nyumbani kwa Mhe. Sophia M. Simba –Masaki Dar es salaam saa 6.00 mchana. Tunawaomba mjumuike nasi.
BWANA
AMETOA NA BWANA AMETWAA,
JINA
LA BWANA LIHIMIDIWE (JOB 1:21)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...