Maendeleo Bank imezindua huduma ya bima ikiwa ni lengo la kuwapatia wateja huduma zote muhimu chini  ya dari moja. Pia inachangia juhudi za serikali kuboresha na kufikisha elimu na huduma za bima kwa wananchi wengi ambao hawajafikiwa. 
Maendeleo Bank Insurance Agency imeanzishwa ili kuunga mkono mkakati wa Serikali wa huduma za kifedha jumuishi ambazo zitahamasisha wananchi wengi watumie na wafikiwe na huduma za kifedha ikiwa ni pamoja na bima. 
 Katika huduma za bima, Maendeleo Bank Insurance Agency imejipanga kutoa huduma zote za bima isipokuwa za maisha. 
Huduma zifuatazo zinapatikana Maendeleo Bank Insurance Agency: Bima za binafsi na za biashara zikiwemo bima za moto na wizi, bima za magari ya aina zote pamoja na mitambo, bima za nyumba na vitu vya majumbani, bima za wafanyakazi, bima za maofisini, bima za biashara, bima za wakandarasi, bima za vitu vinavyosafirishwa na bima za afya. 
 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ‘’Maendeleo Insurance Agency ‘’ Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Ndugu Ibrahim Mwangalaba alisema: 
‘’Kwa kuungana na kampuni ya kimataifa ya Bima yaani, UAP Insurance ni faida kubwa kwa wateja wa Maendeleo Bank Insurance Agency kwani UAP Insurance inauwezo mkubwa wa kubeba bima zote zitakazopelekwa kwao na iwapo itatokea tatizo linalohitaji kugharimia madhara ya kilichowekewa bima, basi mteja wetu hatasumbuka kwani Maendeleo Bank Insurance Agency itafuatilia mambo yote kwa muda mfupi iwezekanavyo ili mteja asisumbuke" Mwangalaba alisema. 
"Bima binafsi au za biashara ni muhimu mno katika kulinda kipato na mali za wateja wetu, uanzishwaji wa huduma za bima ni kuishi kwa vitendo katika kauli mbiu yetu ya pamoja nawe katika maendeleo, kwani tunapenda kuona maendeleo ya wateja wetu yakienda mbele si kurudi nyuma kwa matukio yanayoweza kuzuilika kwa kuwa na bima’’, Mwangalaba aliongezea
  CEO wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba (kulia) na CEO wa UAP Nick Itunga wakipeana mikono baada ya uzinduzi wa Maendleo Insurance agency
 CEO wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba akiongea wakati wa uzinduzi wa Maendeleo Insurance Agency.
Wafanyakazi wa Maendeleo Bank na wa UAP wakiwa katika picha ya Pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...