Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa akikabidhi msaada wa Sukari, kwa Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Abubakari Chalamila kwa ajili ya kituo cha Kitanzani Islamic center kilichoko mjini Iringa.
 Baadhi ya misaada iliyotoa mbunge wa Iringa mjini mch. Peter Msigwa kwa kituo cha  chuo cha Kitanzani Islamic center kilichoko mjini Iringa.  (Picha zote na Denis Mlowe). 
 
Na Denis Mlowe,Iringa
 
MBUNGE wa Iringa Mjini(Chadema) Mchungaji Peter Msigwa amekikabidhi chuo cha Kitanzania Islamic Center msaada wa Sukari,Unga wa Ngano, tende na mafuta ya kupikia ikiwa ni utaratibu wake wa kila mwaka kukisaidia chuo hicho.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo jana kwa Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa Abubakar Chalamila, Mchungaji Msigwa alisema kuwa lengo la kugawa kipindi hiki ni kuwaunga mkono Waislamu katika  mfungo wa Ramadhani na kuwakumbuka wale wote wanaoishi katika mazingira magumu.
 
Mchungaji Msigwa alisema ni jukumu la wadau kuweza kuwasaidia wale wote bila kujali itikadi za vyama kwa kuwa binadamu wote ni wamoja kwa sasa.
 
Mchungaji Msigwa alikabidhi tambi katoni zaidi ya katoni 50, katoni 40 za mafuta ya kupikia, kilo 250 za unga wa ngano na sukari kilo 750 vyote vikiwa na jumla ya thamani zaidi ya shilingi milioni 1.5.
 
Alisema ataendelea kutoa msaada kwa vituo vingine vya watoto yatima na wasiojiweza katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan.
 
Akishukuru kwa msaada huo Kwa niaba ya chuo cha Kitanzani Islamic Center chenye jumla ya wanafunzi 120 ambao wanachukua mafunzo ya dini ya kiislamu Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa, Abubakar Chalamila alisema ni jambo la kujivunia kuwa na mbunge asiyechagua itikadi za dini na mbunge ni akichaguliwa anakuwa wa watu wote bila kubagua watu wake.
 
“Namshukuru sana Msigwa kwa kuweza kutoa msaada huu na  utafikishwa kwa wale wote waliolengwa kupewa na hasa wale wasiojiweza ndio watafaidika na msaada huu wa mbunge wa iringa mjini.” Alisema |Chalamila
 

Chalamila aliwataka wadau wengine kuwakumbuka watu wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu mara kwa mara kwa kuwa ni thawabu kubwa kuweza kuwasaidia. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...