Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini kuendelea  kushikamana kwa lengo la kutekeleza maamrisho ya dini yao  kama inavyoagiza wakati wote. 
Balozi Seif alitoa himizo hilo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada  ya futari ya Pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete kwa ajili  ya Wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba hapo katika Majengo ya  Ikulu ya Mjini Wete,  Pemba
 Balozi Seif alisema njia ya kusimamisha mshikamano kwa  waislam hupatikana katika mjumuisho wa makundi ya ibada, akiyataja kuwa ni pamoja na madrsasa, sala pamoja na  mikusanyiko ya kufutari kwa pamoja. 
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema  kitendo cha Rais Kikwete cha kukutanisha waumini na baadhi  ya wananchi katika maeneo tofauti Nchini kwa ajili ya futari ya pamoja ni moja ya njia ya kuwajengea waumini hao  ushirikiano utakaoongeza mapenzi baina yao. 
 Balozi Seif aliwatakia funga njema pamoja na kusherehekea  kwa amani na upendo siku kuu ya Idd el fitri waumini wote wa  Zanzibar.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa mikoa miwili ya  Pemba Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi  alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.  Jakaya Mrisho Kikwete kwa moyo wake wa kutekeleza ibada  hiyo.
Mh. Dadi alisema mpango huo wa Rais Kikwete ambao pia  hufanywa ba baadhi ya Viongozi wa wengine wa juu hapa  nchini, wakiwemo pia wale wa Taasisi za umma na binafsi  hutoa faraja kwa waumini ambao hali yao ya kipato ni duni  katika kujipatia futari.
Wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba  wakifutari pamoja hapo ikulu ya Wete futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Mauungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho  Kikwete ambaye aliwakilishwa na  Makamu wa Pili wa Rais wa  Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa  Rais wa Zanzibar Mhe Mohamed Aboud Mohamed (katikati)  akiwa pamoja  na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi kulia yake na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa wakijumuika na wananachi wa mikoa miwili ya Pemba kwenye futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi  Seif akitoa shukrani kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya  Muungano wa Tanzania Dr. Kikwete mara baada ya futari ya pamoja kwa wananchi wa mikoa miwili ya Pemba.
 Balozi Seif akiwaaga na baadhi ya wananchi wa mikoa miwili ya pemba waliohudhuria futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete hapo Ikulu ya Wete Pemba.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na  mmoja wa watoto walioshiriki futari ya pamoja iliyoandaliwa  na Rais Dr. Mrisho Kikwete hapo Ikulu ya Wete,  Pemba. Habari na picha na Hassan Issa wa OMPR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2014

    Bwana MICHUZI samahani ikulu ni ya SMZ na sio ya Serikali ya Muungano.Naomba nikurekebishe kidoogo sote ni binaadam sijuwi umeteleza au makusudi lakini ni ya SMZ. Ahsante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...