Bendi Mahiri na Machachari Jijini Dar Skylight Band wametoa wimbo wao wa Tano ikiwa ni muendelezo wa kutoa nyimbo tofauti tofauti kupitia Studio yao ya kisasa ya Skylight Production.
Akiongea na Mtandao huu Meneja wa Band hiyo Aneth Kushaba AK47 amesema wimbo huo unaitwa “Pasua Twende” ambo umetungwa na Mkurugenzi Mkuu wa bendi hiyo Dk. Sebastian Ndege akishirikiana na wanamuziki wa Bendi hiyo.
Aneth akaongezea kwamba wimbo huo ni wa tano kutolewa katika mtiririko wa nyimbo zao zilizokwisha kutoka na imetengenezwa ndani ya studio yao ya Skylight Production chini ya Produzya Joobanjo.
Isikilize hapa chini na Ijumaa hii utapa fursa ya kusikiliza ikipigwa LIVE ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2014

    Hapa Skylight Malaika Band mgefanya guitar la bass kusikika zaidi ya drums, sauti za waimbaji na organ, wimbo huu ungefanya vizuri zaidi na zaidi .

    lakini bado hamjachelewa mtakapotoa video/final edition ya huu wimbo guitar la bass liwe ndiyo linasikika kwa nguvu zaidi bila haja ya Dj au msikilizaji kutumia technolojia kunogesha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...