TIB Development Bank ikishirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imefanya upembuzi yakinifu na kutayarisha michoro kwa ajili ya kuendeleza eneo la ufukweni maarufu kama Coco Beach la jijini Dar es Salaam. 

Mradi huo ujulikanao kama Coco Beach Park utaboresha mazingira na kuongeza vivutio kwenye eneo hilo pendwa kwa wakazi wa Dar es Salaam. Mradi huu utatekelezwa kwa ushirikiano na wabia mbalimbali na utakuwa unamilikiwa na Manispaa ya Kinondoni. 

TIB Development Bank inashirikiana na Manispaa nyingine mbalimbali nchini kutekeleza miradi ya maendeleo mfano Manispaa za Kagera, Moshi, Ilala, Temeke n.k
Mwenyekiti wa Bodi ya TIB Development Bank Profesa William Lyakurwa akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty wakikata utepe kuzindua mradi wa Coco Beach Park. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Development Bank Bwana Peter Noni.
Bwana Jaffar Machano kutoka TIB Development Bank akiielezea michoro ya mradi wa Coco Beach Park kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TIB Profesa William Lyakurwa na Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty
Muonekano wa Coco Beach Park itavyokuwa baada ya kumalizika mradi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2014

    The mdudu zee la kuona mbali,hayo ndio mambo yanayo takiwa na wanachi na mmechelewa mmno kuja na mawazo mazuri kama hayo pongezi sn,,ila msiwe kama yule mama aliejenga bonde la JANGWANI KUANZIA KIGOGO MPAKA YANGA KWA MDOMO pasipo na vitendo kwa mdomo wake alisema atalibadilisha hilo bonde kuwa PARK YA MFANO lakini mpaka leo hakuna chochote.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2014

    Kwikwikwikwi.....Mdudu kweli nami nakumbuka kulikua n maneno kama hayo......na muda ndio huo wayoyoma.......

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2014

    La muhimu zifungwe Kamera ili yule atakaye jisaidia hovyo ama kufanya maujinga yake arushwe live TCB-1 !

    ReplyDelete
  4. Haya ndio maendeleo yanayotakiwa na sio coco tu. Hata Mto Msimbazi ni kitega Uchumi kikubwa sana. Tena leo nimetoa wazo langu jaribu kupitia page yangu katika Facebook inayoitwa Buberwa Robert Blog

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...