Jumuiya ya Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Nchini Korea ya Kusini { KOIKA } imejipanga kuwa kiunganishi kizuri cha wanataaluma wa Korea ya Kusini na wale wa Kitanzania kwa lengo la kudumisha uhusiano uliopo kati ya nchi mbili hizo.

Rais wa KOIKA aliyekuwa kinara wa Ujumbe wa Viongozi Wanne wa Jumuiya hiyo Ndugu Steven Katemba alieleza hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani kwake Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Nd. Steven na ujumbe wake ambao wapo Nchini Tanzania kujitambulisha rasmi baada ya kuchaguliwa kwao kushika dhamana hiyo ya Uongozi wa Jumuiya mnamo Mwezi Mei mwaka huu alisema zipo fursa nyingi za kimasomo na uhusiano Nchini Korea Kusini ambazo Vijana wa Kitanzania wanaweza kuzichangamkia.

Alieleza kwamba Korea ya Kusini iliyopo Bara la Asia ni miongoni mwa Nchi chache za Bara hilo ziliyopiga hatua kubwa za maendeleo na kiuchumi kiasi kwamba Tanzania inaweza kujifunza kupitia maendeleo hayo.

Akitoa Shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Jumuiya hiyo ya Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Nchini Korea Kusini kwa uamuzi wao wa kuunda Jumuiya itakayowasaidia kukabiliana na changa moto zozote zitakazojitokeza mbele yao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliueleza Uongozi wa Jumuiya hiyo ya Koika kwamba uhusiano uliopo kati ya Korea ya Kusini na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni mkubwa na Vijana hao wana haki na wajibu wa kusaidia kuudumisha uhusiano huo muhimu kwa ustawi wa pande zote mbili.
Uongozi wa Jumuiya Watanzania wanaosoma Nchini Korea ya Kusini { KOIKA } ukiongozwa na Rais wake Nd. Steven Katemba ukijitambulisha rasmi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani kwake Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar mara baada ya kucgauliwa rasmi mwezi Mei Mwaka huu. Nyuma ya Ndugu Steven ni Makamu wa Rais wa Jumuiya hiyo kwa upande wa Zanzibar NduguBukheit Juma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaosoma Nchini Korea ya Kusini { KOIKA } uliofika nyumbani kwake kujitambulisha rasmi baada ya kushika wadhifa huo. Kushoito ya Balozi Seif ni Rais wa Jumuiya hiyo ya KOIKA Nd. Steven Katemba na Makamu wa Rais wake Nd. Bukheit Juma. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...