Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) leo Agosti 20,2014 imefanya ziara ya kutembelea Miradi yao ya Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini ili kujionea maendeleo ya ukarabati wa Miradi hiyo miwili ambayo ilikuwa katika ukarabati.Katika ziara hiyo Bodi hiyo ya DAWASA imeridhishwa na upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu chini ambao kwa sasa umekamilika kabisa huku ukiwa na uhakika wa kutoa maji ujazo wa Lita Milioni 270 kwa siku.
Meneja Miradi wa Kampuni ya Megha Engineering & Infrastructures Ltd ya nchini India,Murali Mohan (mwenye kizibao cha kijani) ambao ni wakandarasi wa Ujenzi wa Visima na Ukarabati wa Mabomba ya Maji ya DAWASA katika eneo la Kibamba,akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) ambayo iko chini ya Mwenyekiti wake,Dkt. Eve-Hawa Sinare (wa tatu kushoto) wakati walipopita kwenye Mradi huo utakaosambaza maji kutoka kwenye Mitambo ya Ruvu Juu.Picha zote na Othman Michuzi.
 Meneja Miradi wa Kampuni ya WABAG India,Pintu Dutta (wa pili kushoto) akieleza jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare (wa tatu kushoto) alieambatana na wajumbe wa Bodi hiyo wakati wa ziara yao ya kutembelea Mradi wa Maji wa Ruvu Juu unaonendelea na ukarabati hivi sasa.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare (alienyoosha mkono) akielekeza kitu wakati akiangalia ujenzi wa nyumba za Wafanyakazi wa DAWASA watakaokuwa wanaendesha miradi hiyo ya Maji Ruvu Juu.
 Meneja Miradi wa DAWASA,Ing. Romanus Mwang'ngo (kulia) akiwaonyesha kitu Wajumbe wa Bodi ya DAWASA waliofanya ziara ya kutembelea Mirani ya Ruvu Juu na Ruvu Chini leo Agosti 20,2014.




 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),Alhaji Said El-Maamry (kushoto) akiuliza jambo kwa Meneja Miradi wa DAWASA,Ing. Romanus Mwang'ngo (kulia) juu ya Mtambo wa Ruvu chini,wakati wa ziara yao iliyofanyika leo Agosti 20,2014.Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Dkt. Eve-Hawa Sinare.
Ziara ikiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tokea tumepata Uhuru mpaka leo tumeshindwa kupata wataalam wa maji safi na maji taka,tumeweka wataalam kutoka India.
    Hivi kweli hata hiyo gesi tutaiweza???
    Serikali ijitahidi kutafuta wataalam kwenye sekta muhimu hata kwa kuwasomesha kwa gharama yoyote.
    Hii ni aibu ,tunaomba misaada nchi nje wakati tuna wasomi wanaomaliza kila mwaka.

    ReplyDelete
  2. Usiwe unakurupuka..soma vizuri..huyo ni mkandarasi aliyepewa tenda ya mradi wa upanuzi wa mtambo wa ruvu chini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...