Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira (katikati) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana mjini Dodoma juu ya mkutano wa 30 utakaofanyika nchini mwishoni wiki hii. Kushoto ni Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu Tadesse na kulia ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu Tadesse (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuhusu mkutano wa miaka 30 ya wanahisa na magavana utakao shirikisha nchi 18 za Afrika, mkutano huo utafanyika kesho jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Ofisi ya Rais (Uratibu na Mahusiano), Steven Wasira akifuatiwa na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira (kushoto) abibadilishana mawazo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu Tadesse mara baada ya mkutano na waandishi wa habari jana mjini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA) itakuwa mkutano wa mwaka utakaofanyikia nchini jijini Dar es salaam tarehe 22 mwezi huu.

Hayo yamebainishwa jana mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mkutano huo utakaofanyika mwishoni wiki hii.

“Huu ni mkutano wa kawaida wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa nchi wanachama pamoja na Mawaziri wa Fedha, Tanzania ni mwanachama ndio maana mkutano wa 30 unafanyika hapa” alisema Wasira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...