Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bibi Jacqueline Mneney Maleko akipokea Kompyuta, Vifaa vya Ofisi na Samani kutoka kwa Mwakilishi wa Taasisi ya Marekani ya USAID - East Africa Trade Hub,Bw. Peter Nash. Vifaa hivi ni kwa ajili ya kuanzisha rasmi Ofisi za Kamati za Ushirikiano Mipakani (Joint Border Committees) zilizoanzishwa kwenye mipaka 7 ambayo ni Namanga, Kasumulu, Tunduma, Rusumo, Kabanga, Mtukula na Sirari. Madhumuni yake ni kuimarisha ufanisi wa kupitisha mizigo mipakani na kupata taarifa za biashara mipakani. Tukio hili lilifanyika tarehe 19 Agosti 2014 katika Uwanja wa Mwl. J.K.Nyerere Barabara ya Kilwa, Dar-es-Salaam. Wanaoshuhudia ni Maafisa Waandamizi na Watendaji wa TanTrade. (Picha na TanTrade)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Love you mummy for your hard work and integrity. Keep going you have all of our support. AMaleko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...