Na Rose Masaka,Maelezo
Tanzania imepokea mwongozo mpya juu ya Sheria na Kanuni zinazohusu haki za polisi kumweka
mtuhumiwa chini ya ulinzi na kabla ya kesi kusikilizwa ili kuwapa uelewa wa kutosha wananchi juu ya
haki zao za msingi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Katibu mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Bi.Mary Massay amesema mtuhumiwa anatakiwa kumhoji polisi kosa gani amekamatwa nalo kabla ya
kufikishwa kituoni.
Bi Massay alisema wananchi wengi wamekuwa hawafahamu haki zao za msingi pindi wanapokamatwa
na polisi hivyo kupelekea kuishia magerezani kwa kukosa uelewa wa haki zao za msingi.
Alisema mwongozo huo umepitishwa na Tume za Haki za Binadamu Tanzania, Zimbabwe, Malawi,
Tunisia na Ivory Coast na unahusu utendaji wa polisi ambapo unawataka wananchi wa Tanzania
kutambua haki zao za msingi pindi wanapokamatwa na polisi.
Akifungua mkutano huo mwandishi maalumu wa wafungwa na mazingira Kamishna Med Kaggwa
kutoka taasisi ya Haki za Binadamu Uganda aliongeza kuwa Afrika inahitaji ushauri ili iweze kufanya
kazi zake kwa ufanisi kwa sababu kuna maeneo mengi ya kisheria ambayo yanatakiwa kufanyiwa
marekebisho.
Kamishna Kaggwa alisema mtuhumiwa kufungwa kabla ya uchunguzi kukamilika ni ukiukwaji wa
sheria hivyo polisi wanatakiwa kufuata na kuheshimu sheria na kanuni zilizotungwa na nchi.
Alisema kutokana na utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa asilimia 41.3 ya wafungwa wa Afrika hukuo
afrika kusini ikiwa na wafungwa wengi zaidi,na asilimia 50 ya wafungwa wa Tanzania ni wafungwa wa
muda mchache kati ya miaka 3 hadi 4 kupata hukumu.
Mwandishi Maalumu wa Wafungwa Bw. Med Kaggwa kutoka Taasisi ya Haki za
Binadamu ya Uganda aliyesimama akifungua Warsha ya siku mbili juu ya mwongozo mpya wa
Sheria na Kanuni za polisi kumweka mtuhumiwa chini ya ulinzi na kabla ya kusikilizwa.warsha
hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Bi. Louise Edward kutoka Taasisi ya “African Policing Civilian Oversight Forum
(APCOF) akitoa mada katika Warsha ya siku mbili juu ya mwongozo mpya wa Sheria na Kanuni
za polisi kumweka mtuhumiwa chini ya ulinzi na kabla ya kusikilizwa.warsha hiyo imefanyika
jijini Dar es Salaam leo.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja katika Warsha ya siku mbili juu ya
mwongozo mpya wa Sheria na Kanuni za polisi kumweka mtuhumiwa chini ya ulinzi na kabla
ya kusikilizwa.warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Picha zote na Benjamin Sawe wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHVUM
KWA UELEWA WANGU MTOA HAKI ANATAKIA ATOE HAKI HATA KABLA ANAYEPEWA HAKI HAJAIULIZIA. KWA HIYO POLISI WATOE HAKI YA RAIA HATA KAMA HUYO RAIA HAJUI HAKI YAKE. HAIMANIISHI KWAMBA MTU ASIPOJUA HAKI YAKE NDIYO ANYIMWE HAKI YAKE; HII SI KWELI. TUJITAHIDI WANANCHI WENZANGU KUTOA HAKI AMBAYO IKO CHINI YA USIMAMIZI WAKO KWA MHUSIKA HATA KABLA MHUSIKA HAJAIOMBA. KAZI NJEMA KAKA MICHUZI.
ReplyDeleteUKO SAHIHI SANA MKUU WANGU HAPO JUU....KAMA VILE AMBAVYO KUTOJUA SHERIA HAKUMPI "EXCUSE" ALIYETENDA KOSA....KADHALIKA KUTOJUA HAKI HAKUPASWI KUMFANYA ANAYEJUA HAKI ASIMPE ASIYEJUA HAKI, HAKI YAKE...TUKIUFIKIA UPEO HUO WA USTAARABU TAIFA LITAKUWA LINASHUHUDIA JAMII YA KISTAARABU SANA HAPA KWETU TZ.
ReplyDelete