Mtaalam wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kutoka kituo cha mazingira cha Finland akitoa maelezo kwa baadhi ya viongozi wa Tanzania kuhusu htu zinazochukuliwa na nchi hiyo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
 Viongozi wa Tanzania wakiwemo mameya na wakurugenzi wa majiji sita ya Tanzania walioko nchini Finland kwa ziara ya mafunzo inayoratibiwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania wakipata maelezo kuhusu aina mpya ya gari inayoendeshwa kwa kutumia umeme iliyoko katika kituo cha mazingira cha Finland kiitwacho Helsinki Environmental centre.

Na Vedasto Msungu wa ITV Finland

Viongozi wa wa Tanzania wakiwemo mameya na wakurugenzi wa majiji sita ya Tanzania walioko katika ziara ya mafunzo nchini Finland wametembelea kituo cha mazingira cha nchi hiyo kiitwacho Helsinki Environmetal centre kujifunza kuhusu hatua zinazochukuliwa na nchi hiyo kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabianchi.

Wakongea na viongozi hao kutoka majiji sita ya Tanzania ikiwemo Dar Es salaam, Mbeya, Mwanza, Arusha, Tanga na Zanzibar, watendaji wa kituo hicho wamesema nchi hiyo imeanza kuchukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabianchi.

Wamezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kutilia mkazo suala la upandaji miti lakini pia kumeanzishwa mpango wa matumizi ya magari yasiyohitaji kutumia mafuyt ya dizeli au petrol ambayo sasa yanaendeshwa kwa kutumia umeme.

Kwa mujibu wa wataalam wa mazingira wa kituo hicho, hatua hizo zinalenga kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa unaotokana na ongezeko la shughuli za binadamu ikiwemo moshi wa viwanda, magari na ukataji miti ovyo.Wamesema matumizi ya magari hayo yanayoendeshwa kwa kutumia umeme yanaendelea kuongezeka na kwamba katika nchi hiyo kuna vituo zaidi ya 50 vya kuchaji magari hayo kwa umeme na pia kila raia wa Finland anaemiliki gari ya aina hiyo anaweza kuchaji gari nyumbani kwake.

Aidha wametaja matumizi ya vioo vya madirisha au milango ambayo imewekwa vioo maalum vinavyofungwa kwenye madirisha au milango lakini wakati huo huo ni panel za sola zinazozalisha umeme na kutumika kw shughuli mbalimbali ikiwemo viwandani na majumbani.

Wametaja mfano katika jingo lao kuwa panel za sola zilizoko kwenye milango na madirisha zinazalisha umeme mwingi ambao hutumika kwa shughuli za ofisi na unaobaki unaingizwa katika gridi ya taifa kwaajili ya watumiaji wengine.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Gari za umeme siyo mpya, zlishakuwepo miaka mingi tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...