Balozi Tuvako Manongi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sita ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, akimkaribisha Rais wa Baraza Kuu la 69 la Umoja wa Mataifa, Bw. Sam Kutesa ( wa kwanza kushoto) kuzungumza na wajumbe wa Kamati hiyo ya Sita ambayo jukumu lake ni kuratibu na kuendesha mijadala yote inayohusu masuala ya sheria. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa kipindi cha mwaka moja. Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amekuwa akitembelea na kuzungumza na wajumbe wa Kamati Sita ambazo ziko nchini ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kamati hizo ni, Kamati ya kwanza inayohusika na masuala ya Upokonyaji wa Silaha na Usalama wa Kimataifa, Kamati ya Pili inahusika na masuala ya Uchumi na Fedha, Kamati ya Tatu yenyewe inahusika na masuala yote yanayohusu Jamii, Hakiza Binadamu na Utamaduni, Kamati ya Nne inahusika na masuala ya Siasa na umalizaji wa ukoloni. Ili hali Kamati ya Tano inahusika na masuala ya Utawala na Bajeti na Kamati ya Sita inahusu masuala ya sheria.
Wajumbe wa Kamati ya Sita ambayo iko chini ya Uenyekiti wa Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakimsikiliza Rais wa Baraza Kuu la 69 la Umoja wa Mataifa, Bw. Sam Kutesa ambaye amewataka wajumbe wa kamati hiyo kuendesha mijadala ya ajenda zao kwa kuzingatia taratibu walizojiwekea ili hatimaye waweza kupitisha maazimio na maamuzi kwa kauli moja. Akasema ofisi yake itakuwa tayari kutoa ushirikiano wa karibu kwa Kamati hiyo na akampongeza Mwenyekiti kwa namna ambavyo amekuwa akiendesha na kusimamia shughuli za Kamati .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...