Basi la Simba mtoto linalofanya safari zake kati ya Dar na Tanga likiwa limegongana uso kwa uso na Lori la mizigo katikati ya Daraja la Mto Wami mkoani Pwani,dereva wa lori hilo amefariki papo hapo na wengine kujeruhiwa.tutaendelea kupeana taarifa zaidi hapo baadae.
Baadhi ya wasamaria wema wakijaribu kumchomoa Dereva wa Lori hilo aliyekuwa amebanwa vibaya,pichani ambalo namba zake za usajili hazikufahamika mara moja.
Kwa haraka tu inawezekana hilo lori lilikatika break....otherwise madereva wote walikuwa wamekunywa au wana akili yao mbovu...
ReplyDeleteSiyo rahisi kuamini kutokea kwa ajali kama hiyo hapo darajani. ni wazi kuna uzembe mkubwa wa madereva waliohusika na ajari hiyo. mahali kama hapo huwa panakuwa na speed ndogo kama 30km/h hivi ambayo haingeweza kusababisha ajari mbaya na kuua watu.
ReplyDeleteHizi ajali zinatisha
ReplyDeleteIla Tanzania kweli ee kweli. Inawezekanaje ajali itokee darajani jamani? kweli? sasa na daraja la kigamboni si ndio watu wataishia bahari ya hindi? mie nipo hapa. Anyway, pole sana majeruhi na waliofariki wapumzike kwa amani ya bwana. This is too much Tanzania.
ReplyDeleteKawaida bongo,same stuff everyday
ReplyDeleteMadereva nendeni mukasomee udereva ili mujue sheria za barabara
ReplyDeleteJamani hata siamini kilichotokea. Huu ni uzembe wa madereva kutokuwa makini na vyombo vya moto hadi kutokuwa na umakina kama wamebeba roho za watu...Embu ona sasa can you imagine? Yaani ....
ReplyDeletehapo itakuwa umefanyika uzembe wa hali ya juu hawakutaka kusubiriana kwani hapo inaingia gari moja tuu.
ReplyDeleteNyingine inatakiwa kusubiri aonekweupe ndio aingie.
Kwakweli daraja la wami linabidi liongezwe upana kwani ni laenzi za wakoloni, inakuwa vigumu kwa magari makubwa kupishana
ReplyDeleteIVI KWELI KTK ULIMWENGU HUU TULIOKUA NAO SASA AJARI ZA KUGONGANA USO KWA USO ZIPO KWELI??KWELI TZ SOKOMOKO OVYOOOO YAANI SIPATI PICHA....HILI SI SUALA LA HAO WALIOPATA AJARI TU KUNA WENGI WANAINGIA HAPA....NI TAABU TUPU....
ReplyDeleteHII INAONYESHA JINSI WATU HAWAJALI UHAI WAO, KWASABABU HII NI AJALI AMBAYO IMETENGENEZWA MAKUSUDI, DARAJA LA WAMI HUWEZI KUKOSA KUMWONA MWENZIO ANAEKUJA MBELE YAKO ILIKUWAJE MPAKA UINGIE DARAJSANI WAKATI MWENZIO UNAMWONA AMESHAINGIA KWENYE HILO DARAJA JAMBAMBA NA WEWE UNAINGIA TU.
ReplyDeleteWaswahili tunasema: Ajali haina kinga!!! How dumb!
ReplyDeleteNi bola daraja hili magufuri alitanue au viwekwe vizuizi vya kusubiliana mwazoni mwa daraja
ReplyDeleteSi sahihi kuyaita matukio haya Ajali. Haya ni mauaji ya barabarani.
ReplyDelete