Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Barnabas Ndunguru
akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (hayupo Pichani) katika ufungaji wa
mafunzo elekezi kwa watumishi wapya wa Wizara.Hafla hiyo ilifanyika hivi
karibuni jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi
Sihaba Nkinga akiongea na baadhi ya Watumishi wapya wa Wizara katika ufungaji
wa mafunzo elekezi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo aliwaasa kuwa na
maadili katika utendaji wao wa kazi.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi
Sihaba Nkinga katikati akiongea na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw.
Leonard Thadeo kulia na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Prof.
Hermens Mwansoko kushoto mara baada ya kufunga mafunzo elekezi kwa
watumishi wapya wa Wizara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...