Kikosi cha Kiluvya United kikifanya mazoezi mepesi kabla ya mechi yao ya Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 katika Uwanja wa Makurumla dhidi ya Sinza Star. Kiluvya United ilishinda 3-0.
 Wachezaji wa Sinza Star wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mchezo wao na Kiluvya United.
 Wachezaji wa Kiluvya United wakisalimiana na wachezaji wa Sinza Stara kabla ya mchezo wao wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Makurumla jijini Dar es Salaam. Kiluvya United ilishinda 3-0 na kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. 
 Kikosi cha Kiluvya United kikiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi kamili cha timu ya Snza Star kikiwa katika picha ya pamoja.
Beki wa tmu ya Kiluvya United, Mwita Enoshi (kushoto) akiwania mpira na mshambuliaji wa Sinza Stars katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Makurumla Dar es Salaam. Kiluvya ilishinda 3-0 na kutinga hatua ya robo fainali ya mchuano hiyo.
Mshambuliaji wa timu ya Kiluvya United, Haji Zege (kushoto) akichuana na beki wa Sinza Stars Charles Kaembe katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Makurumla Dar es Salaam. Kiluvya ilishinda 3-0 na kutinga hatua ya robo fainali ya mchuano hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...