Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Nd. Abdullah Juma Abdullah kuchukuwa hatua ya kuyapeleka TRA Makontena yote yaliyoshindwa kufuata tataribu ambayo yanaleta msongamano ndani ya Bandari hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Nd. Abdullah Juma Abdullah akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baadhi ya maeneo yaliyowekwa makontena ndani ya Bandari hiyo.
Balozi Seif alifanya ziara ya ghafla ndani ya Bandari hiyo ili kujionea hali halisi ya utendaji wa bandari ya Malindi,Zanzibar.
Mrundikano mkubwa wa makontena unaoonekana katika Bandari ya Malindi ambapo baadhi ya wafanyabiashara wanashindwa kutoa makontena yao na kuleta usumbufu kwa watendaji wa Bandari hiyo.Picha na – OMPR – ZNZ.
Njia nyingine ya kupunguza msongamano bandarini ni kutenga maeneo mengine ya hifadhi za mizigo mjini nje ya bandari.
ReplyDelete