SIKU mbili  baada ya kufungashiwa virago vyao kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika, uongzi wa Azam umefumua benchi lake la ufundi na kumtupia virago kocha wao Joseph Omong.

Katika taarifa ya uongozi huo waliyotoa jioni jioni hii,uongozi huo haujatoa sababu yoyote  ya kuachana na Omong ambaye wamekuwa nae kwa miezi 14.

Hata hivyo habari ambazo Globu ya Jamii imezipata zinasema kuwa uongozi wa Azam umeamua kumtupia virago Omong kutokana na kufanya vibaya kwenye michuano ya Klabu bingwa Afrika baada ya kunyukwa mabao 3-0 na El Merreikh  ya Sudan Jumamosi ya mwishoni mwa wiki iliyopita na hivyo kutolewa kwa jumla y a mabao 3-2.

Katika michuano hiyo Azam ilienda Sudan ikiwa na hazina ya mabao 2-0 iliyopata katika mechi ya  kwanza wiki mbili zilizopita, lakini wenyeji walitumia nafasi ya kucheza nyumbani na Azam kuaga mashindano.

Omog ambaye anaicha Azam ikiwa nafasi ya pili katika msimammo wa Ligi ikiwa imecheza mechi 15 imeshinda saba, imetoa sare sita na kupoteza miwili, aliiwezesha  Azam  kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza  msimu uliopita, na leo ametimuliwa na msaidizi wake  Ibrahim Shikanda.

Kikosi hicho cha wana lamba lamba  kitaongozwa na Kocha msaidizi  George Best Nsimbe kuikabili JKT Ruvu Jumamosi ijayo katika mechi ya Ligi itakayochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex.

Kutimuliwa kwa makocha hao ni mwendelezo wa timua timua ndani ya Azam ambayo awali katika msimu wake wa kwanza ligi kuu, Azam ikiwa bado inaundwa na wachezaji wengi waliopandishwa timu, ilimfukuza Neider dos Santos baada ya kufungwa na Simba ikawa chini ya Itamar Amorin.
Itamar aliondoka kwa sababu ya kuzidiwa nguvu na wachezaji wasio na nidhamu mbele ya uongozi timu akakabidhiwa Stewart  Hall mara ya kwanza aliondolewa tu katika mazingira ambayo hayakueleweka, walimchoka tu na wakamwajiri Boris Bunjak raia wa Serbia
  
Mserbia huyo naye, pamoja na kuiongoza vizuri timu ikiwa kwenye mbio za ubingwa hadi mwishoni mwa mzunguko wa kwanza, baada ya kufungwa na Simba naye akafukuzwa. Akarudi Stewart na akafanikiwa kuzifunga Simba na Yanga katika msimu wa 2013/2014, lakini haikutosha baada ya mzunguko wa kwanza, akaambiwa aondoke. Timu hiyo ikakabidhiwa mikoni mwa Omong ambaye ameiongoza kwa miezi 14 na hatma yake ndani ya klabu hiyo imehitimishwa jana kwa kupewa mkono wa kwaheri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. alistahili kufukuzwa kwa sababu moja uongozi wa azam ulimpa kocha kila kitu maandalizi ya azam walieka kambi karibu nchi tatu LKN MPIRA WA AZAM ULIKUWA WA CHINI SANA WACHEZAJI WA AZAM WALIKUW wanacheza kwa uwezo wao binafsi mm naona kastahili kufukuzwa rabda wachezaji walikuwa hawamuelewi au hawamtaki

    ReplyDelete
  2. mtabadili bucha tu nyama ile ile!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...