MKUTANO Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), pamoja na klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza, uliofanyika Februali 28, mwaka huu,  umejadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja msimu ujao wa Ligi Daraja la kwanza kupata udhamini.

 Kaimu Mtendaji wa Bodi hiyo Fatma Shibo, alisema kuwa katika mkutano huo, kulijadiliwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na utendaji wa bodi hiyo.

Alisema kuwa moja ya vitu vilivyojadiliwa ni vurugu za zinazotokea viwanjani, maoni ya klabu kuhusu viwanja vinavyotumika kwa ligi hizo.

Shibo alisema kuwa klabu za ligi kuu zililalamikia mfomu wa tiketi za Kieletroniki, ambapo klabu zimelalamikia mapato kupungua kwa asilimia 40.

Alisema Bodi ya ligi imelichukua hilo na kulifanyia kazi kwakuwa ilikuwa tayari imeanza mazungumzo na kampuni inayohusika na utengezwaji wa Tiketi ya CRDB, mapmoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzani (TFF).

Shibo alisema kuwa katika mkutano huo klabu za ligi daraja la kwanza nao zimepata mdhamini ambaye ni kampuni ya TV ya Azam Tv, ambayo, msimu ujao itakuwa inaonesha mechi za.

Katika suala la malalamiko ya waamuzi, tayari kamati ya utendaji ya TFF, iliteuwa kamati maalum, ambayo itakuwa ikifuatilia na kutoa maamuzi ndani ya masaa 75.

Alisema kamati hiyo imemteuwa Said Mohamed, ambaye ni mwenyekiti  wakati makamu wake ni Geofrey Nyange Kaburu, wajumbe ni Charles Ndfagala na Steven Mguto.

"Katika mkutano huo suala la waamuzi na tiketi zilichukua nafasi kubwa kwa sababu klabu zinadai mapato kupungua kwa asilia 40, hivyo bodi ya ligi, TFF na CRDB, tunaendelea kufanya vikao, vya kutatua tatizo hilo"alisema Shibo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...