Taasisi ya Vodafone Foundation leo imetangaza kuwa mpango wake wa kutoa elimu kidigitali umewezesha jamii zinazoishi kwenye mazingira magumu yanayosababishwa na majanga mbalimbali na  kujikuta zikiishi kwenye kambi za wakimbizi kuweza  kupata elimu.

Mpango huu wa   unatekelezwa katika  maeneo yenye mazingira magumu ambako kuna matatizo ya kutokuwepo nishati ya umeme na  upatikanaji wa mawasiliano hususani ya mtandao wa interneti na umeweza kutekelezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

Ufunguzi wa madarasa chini ya mpango huu unafanyika kwa kutumia masanduku maalum yanayobeba vifaa vya kufundishia ,kuzalisha nishati ya umeme,kuchaji vifaa vya kufundishia na modemu maalumu za interneti ambazo hazihitaji kuunganishwa papo kwa papo .Vifaa vyote hivi vilivyoandaliwa kwa ajili ya mpango huu  unaoendeshwa kwenye maeneo yenye mazingira magumu vikiunganishwa kwa muda mfupi vinawezesha walimu maalumu walioandaliwa kuvitumia kuweza kuwapatia elimu wanafunzi bila matatizo yoyote.


Masanduku  maalumu ya kubeba vifaa vinavyotumika kutolea elimu hili yameandaliwa kutumika kuchaji vifaa vyote na vikishawekwa kwenye chaji kwa muda wa kati ya masaa 6-8 sanduku linaweza kutumika siku nzima kufundishia bila kuhitaji nishati ya umeme.


Mpaka mwaka ujao mpango huu utakuwa umetekelezwa katika shule 12 kwenye makambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya,Nyarugusu nchini Tanzania na Demokrasia ya Congo na utatoa elimu bora kwa watoto wapatao 15,000 wenye umri kati ya miaka 7 -20 .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...