Waziri wa Utalii na Maliasili Razalo Nyarandu akitoa nasaha za kuwaaga wafanyabiashara wa Tanzaia wanaoenda Berlin Ujerumani
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akitoa nasaha za kuwaaga wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda Berlin, Ujerumani kushiriki maonyesho makubwa Duniani ya biashara maarufu kama ITB kuanzia Machi 4-8 mwaka huu.

Na Andrew Chale.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewataka wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda kushiriki maonyesho makubwa Duniani ya biashara maarufu kama ITB, mjini Berlin, Ujerumani Machi 4 hadi 8, mwaka huu, kubeba uzalendo na kuitangaza Tanzania hususani vivutio vya Utalii na utajiri wa maliasili ili kuvutia wawekezaji.

Nyalandu aliyasema hayo usiku wa Februari 27, wakati wa halfa fupi ya kuwaaga wafanyabiashara hao ambapo alisema kuwa, kwenda kwao huko kushiriki maonyesho hayo makubwa kabisa duniani, ni fursa kama Tanzania kupata kujitangaza zaidi na kuvutia wawekezaji.
DSC_0151
Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...