Innalillahi wa Inna Ilaihi Rajioun:SUPREME Mufti wa Uganda  ambaye pia ni Murshid wa Twariqatus-Shaadhuliy nchini Uganda, Sidi. Sheikh Zubeir Kayongo amefariki dunia katika hospitali ya Agha Khan Jijini , Dar es salaam jana alikokuwa amelazwa muda mfupi akiwa  njiani kuelekeya Kilwa Pande kuhudhuria HAUL na Ziyarah  ya kutimiza  miaka 100 ya Sidi.Sheikh Muhammad Al- Maaruf As-Shadhuly(QAS).

Marehemu aliwahi kuhudhuria Ziyarah ya Mawlid  Jijini  Unguja Mfunguo 6. na Twariqatul Shaadhuliya nchini humo ilimfanyiya hadhra maalum kwa heshima yake katika  Msikiti wa Mwembetanga Jijini Unguja.Ilikuwa ni desturi ya .Al-Marhum SUPREME Mufti wa Uganda  kila mwaka  kuhudhuria Hawl ya Sheikhe Muhammad Al Maarufu aliyeleta Twariqatu Shadhuliyah Afrika ya Masharika mwanzoni mwa miaka ya 1900 toka huko Akka Palestina inayokaliwa kwa Mabavu alipochukua Twariqah hiyo toka kwa Sheikhe lake Sidi Sheikh.

Ali Nurdin Al-Yashurutwi(QAS).Twariqah ya Shadhuli imeenea maeneo mengi duniani ikiwemo Uganda ambapo ilifika miaka ya mwanzoni mwa 1900 chini ya Sidi.Sheikh.Hussein Ibn Hussein wa Kilwa Pande aliyepokea Twariqah toka kwa Sidi Sheikh Muhammad Al-Maarufu wa Ngazija.

Nchi zingine zilizoenea Twariqah hii ni  Misr, Morocco(Maghreb), Algeria,Tunisia, Sudan, Sri-Lanka, India, Pakistani, Jerusalem(Palestina),Libya, Uingereza, America, Canada, Australia, Afrika Mashariki na mwanzilishi wa Twariqah hii akitokea huko Morocco na aliyetawafu huko nchini Misri akielekea safari ya Hajj  kwa umaarufu akiitwa Sidi.


Sheikh Abal Hassan As-Shadhuly, Jina la Shadhuly linatokana na mji wa huko Afriqiyah(Tunis) ambako ndipo harakati za Sheikhe zilipoanzia kueneza Daawah ya Kitwariqah yenye kushikamana na Quraan na Sunnah kwa mujibu wa mafundisho ya Ahlul Sunnah walJamaa..


Watu wengine maarufu waliokuwa wakifuata Twariqah hii ni Imam alHafidh  Jalaludin As-Suyutwi aliyekuwa mufasir maaruf wa Quraan na Hadith (Tafsir Jalalayn),Sidi Sheikh Umar Mukhtar As-Sanusi(mwanaharakati wa Ki-Libya maarufu kama The Lion of The Desert), Shahidi.Sidi.Sheikh Hassan Al-Bannah(Rahimahullah) mwanzilishi wa harakati Ikhwaan Al- Muslimun  ya nchini  Misri, aliyekuwa Mfalme wa Libya Mfalme  Idriss   aliyepinduliwa na Kanali Muammar  Gadafi   Wengine katika karne ya sasa ni wanachuoni wakubwa wa Hadith huko Maghreb wajulikanao kama Saadah al-Ghumari ,, Mwanachuoni wa Hadith wa Alexandria Al-Kahtan, pia aliekuwa Mufti wa nchi ya Misr, Sidi.Sheikh Dr.Ali Gumua na Maulamaa wengine wengi wa Al-Azhari Shariyf na Qarawiyin University  huko Maghreb ni Murshid wa Twariqah hii ya Shadhuly..Tunamuomba Mola Amjaalie Mayiti wetu Sheikhe letu Sidi.Sheikh Zuberi Kayongo msamaha wa mapungufu yake na Amjaalie Mayiti wetu pepo iliyo juu kabisa na tunamuomba Mola amtakase mayiti wetu kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na madhambi yake na amjaalie kaburi lake liwe ni katika viwanja vya pepo , Tunamuomba Mola wetu ampe majazo mema kutokamana na amali zinazoendelea na zile zitakazofanywa kwa niaba yake iwe na mimea au viumbe katika wanadamu,Malaika na Majini Yaa Raab.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Inna lillahi wa Inna ilayhi rrajiuun.

    Mwenyezi Mungu ampe makazi mema peponi apokewe kwa furaha na amani.

    Aaamin

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...