Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

BOHARI ya dawa (MSD) imeboresha huduma kwa wateja wake kwa kutoa taarifa zinazomhusu mteja kwa kuziweka wazi katika tovuti yao.

Amesema hayo Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na Shughuli za Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry, akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.

Terry amesema kuwa taarifa hizo ni za mali inayopatikanagharani, taarifa za kiasi cha fedha za wateja kilichopo katika kila akaunti,fomu za marejesho pamoja na bei za bidhaa na bei zake.

Pia Terry amesema kuwa wateja wenye mahitaji ya dawa au vifaa wanatakiwa kuandika barua kuelezea mahitaji yao pamoja na maelekezo mhimu ya kifaa husika na kutatuliwa na kitengo cha manunuzi ya bohari hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda Bohari ya dawa (MSD), Edward Terry,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa habari MAELEZO jijjini Dar es Salaam leo kuhusu utendaji na mipango ya Bohari ya Dawa (MSD) na Ofisa Uhusiano Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),Etty Kusiluka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...