Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
JAMII imeaswa kuunga mkono juhudi mbalimbali dhidi ya mapambano  ya ukosefu lishe bora  kutokana na kudumaza watoto na kushindwa taifa kupata nguvu kazi katika jitihada za kusukuma uchumi.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Masuala ya Lishe pamoja na Haki za Watoto,Lediana Mng’ong’o wakati akizindua ripoti lishe Duniani iliyokutanisha nchi mbalimbali kwa ajili ya kuweza kupata nguvu katika kupambana na lishe, iliyofanyika leo katika Hoteli ya Protea, Jijini Dar es Salaam.

Lediana amesema kuwa katika mapambano ya lishe inahitajika  kuwa na  sauti moja katika kuzungumzia suala hilo ikiwa ni pamoja na kushirikisha viongozi wa vyama pamoja wabunge.

Amesema suala hili likipewa utashi wa kisiasa kama yeye alivyojitoa katika mapambano na jitihada za watu wengine kuna uwezekano wa kupunguza tatizo la lishe lililopo sasa.

Aidha amesema hali ya lishe kwa mwaka 2010 watato waliodumaa kwa lishe ilikuwa asilimia 42 lakini kutokana na jitihada za mapambano hayo imefikia asilimia 35.

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Lishe Tanzania(PANITA),Tumaini Mikindo amesema kuwa sasa ni wakati wa kuweka mkazo wa kuwepo bajeti za masuala ya lishe kuanzia katika ngazi ya kata katika kupunguza utapiamlo.

 Amesema kutokana na ripoti hiyo na wadau walioshiriki wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa ni hatua nyingine katika kuongeza kasi dhidi ya mapambano ya lishe nchini.
  Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Masuala ya Lishe pamoja na Haki za Watoto,Lediana Mng’ong’o akizungumza na wadau wa masuala ya lishe kwa watoto wakati wa kuzindua ripoti ya masuala ya lishe Duniani katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi  Mkuu wa ushirikiano wa lishe Tanzania (PANITA), Tumaini Mikindo akifafanua jambo katika uzindua wa Ripoti ya masuala ya lishe Duniani  leo katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi  Mkuu wa ushirikiano wa lishe Tanzania (PANITA), Tumaini Mikindo akifafanua jambo katika uzindua wa Ripoti ya masuala ya lishe Duniani leo katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa masuala ya lishe nchini Burundi, Jean Nkurunziza akitoa mchango wake kuhusiana na masuala ya  lishe nchini Burundi katika mkutano wa kuzindua ripoti ya masuala ya lishe Duniani iliyofanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za watoto Tanzania(TAJOC),Chalila Kibuda akiweka saini juu ya mapambano ya lishe katika uzinduzi wa ripoti ya Lishe Duniani iliyofanyika leo katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
Wadau wa lishe wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wameshika Ripoti ya Lishe Duniani mara baada ya kutoka katika mkutano wa uzinduzi wa Ripoti hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2015

    Kampeni za chakula bora, chanjo, elimu ya watu wazima, na uchimbaji vyoo au mtu ni afya zilikuwepo toka miaka ya sabini zianzishwe upya na taasisi husika katika kila wilaya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...