Wadhamini
wakuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania imetangaza rasmi zawadi zitakazotolewa hivi karibuni
kwa Mabingwa wa ligi hiyo iliyomalizika hivi karibuni ambapo
timu ya Yanga yenye makazi yake Jangwani jijini Dar es Salaam iliibuka
na ubingwa.
Kwa
mujibu wa mkataba wa ligi na mdhamini mbali na zawadi kutolewa kwa timu
bingwa zimekuwa zikitolewa pia kwa,mshindi wa pili na wa tatu katika
ligi,mfungaji bora,timu iliyoonyesha nidhamu,mchezaji bora wa mwezi
na wa ligi nzima,refa bora , kocha bora na golikipa bora.
Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amethibitisha kuwa fungu
nono litakalokabidhiwa kwa mabingwa na ambapo alisema kimeongezeka
kiasi cha milioni 13 tofauti na mkataba wa awali.
“Kama
inavyojulikana kuwa thamani ya shilingi imeshuka hivyo kama wadhamini
tumelazimika kuongeza fedha za zawadi ili ziendane na wakati na lengo
kubwa ni kuongeza motisha kwenye ligi hii kubwa ya soka nchini
ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikidhaminiwa na kampuni ya Vodacom”.
Alizitaja zawadi timu bingwa itapata shilingi
80,401,160/-
tofauti na 75,565,000/- za awali,mshindi wa pili shilingi 40,200,580/-
awali zilikuwa 37,782,500/-,mshindi wa tatu shilingi 28,714,700/-
awali zilikuwa shilingi
26,987,5000/-,mshindi wa nne shilingi 22,971,760 awali zilikuwa
shilingi 21,590,000/-,mfungaji bora shilingi 5,742,940/- ambapo awali
ilikuwa 5,397,500/-,golikipa bora shilingi 5,742,940/- awali ilikuwa
shilingi 5,397,500/-,timu iliyoongoza kwa nidhamu bora
shilingi 17,228,820/- awali ilikuwa 16,192,500/-,Mchezaji bora wa msimu
wa 2014/2015 shilingi 5,742,940/- ambapo awali ilikuwa 5,397,500/-,Refa
bora shilingi 8,614,410/- awali ilikuwa 8,096,250/-na kocha bora
shilingi 8,614,410/- ambapo awali ilikuwa 8,096,250/-pia
kuna zawadi ya milioni 9,000,000/- ambapo kila mchezaji bora wa mwezi
alikuwa akizawadiwa milioni 1,000,000/katika kipindi cha miaka 9
Alisema baada ya kumalizika ligi mchakato unafanyika wa kukabidi zawadi katika siku za karibu. “Katika siku chache zijazo tutawakabidhi washindi na wadau wote waliofanya vizuri na tunajivunia kuona ligi hii
inazidi kuwa na msisimko mwaka hadi mwaka”.
Alipoulizwa mipango ya kampuni iwapo itaendelea kudhamini ligi hiyo alisema
ninapenda kuwahakikishia wapenzi wa soka nchini wasiwe na wasiwasi kuhusiana na suala la sisi kuendelea kuwa wadhamini kwani
kwasasa bado tupo mezani kwa mazungumzo ya kina na TFF kujua nini
tukiboreshe kwa msimu ujao na wapi tulikokosea msimu huu uliopita kwa
kifupi hakuna kitakachoharibika muda ukifika tutawajulisha,Alisema Nkurlu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...