Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2015/2016 bungeni leo mjini Dodoma.  Mabalozi wa Tanzania kwenye nchi mbalimbali duniani wakifuatilia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka 2015/2016 iliyowasilishwa leo bungeni mjini Dodoma. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Harrison Mwakyembe akimsikiliza kwa makini mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere (kushoto) nje ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma. Kulia ni mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. ShyRose Bhanji. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju (kulia) akisisitiza jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma jana.  Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Harrison Mwakyembe akifurahia jambo na wabunge wa bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere (kushoto) na Mhe. ShyRose Bhanji (kulia) mara baada ya kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2015/2016  leo bungeni mjini Dodoma. PICHA ZOTE NA FATMA SALUM - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...