Klabu
ya Kimondo Super Sports inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania yenye
maskani yake wilayani Mbozi mkoani Mbeya inapenda kutoa tamko juu ya mkanganganyiko wa
taarifa za kuptosha za usajili wa mchezaji wake Geofrey Bahati Mwashiuya.
Klabu
inasikitishwa saana na habari/taarifa zenye mkanganyiko zinazotolewa na msemaji
wa timu ya Yanga,Katibu wa timu ya Yanga na mchezaji wetu Geofrey Mwashiuya
katika vyombo mbalimbali vya habari;
Jerry
Muro alisikika katika vyombo vya habari akijinadi kuwa klabu ya soka ya Yanga
imemsajili Geofrey Mwashiuya tangu Oktoba,2014 kwa kandarasi ya miaka
mitatu,wakati huohuo Katibu wa Yanga Dkt,Jonas Tiboroha alidai mchezaji huyu
alisajiliwa na klabu ya Yanga tangu mwezi Februari,2015.
Klabu
ya KIMONDO inasikitishwa na taarifa hizi zenye mkanganyiko mkubwa kuhusu suala
la mchezaji huyu,na kwa kauli hizo mbili zinazokinzana Watanzania wanaweza
kuona ukweli wa mambo ukoje.
Taarifa
sahihi ni kwamba mchezaji Geofrey Mwashiuya ana mkataba wa miaka minne na timu
yetu ya KIMONDO na ndio muda sahihi
ulioandikwa katika TMS na uliopo katika mkataba wa maandishi. Zaidi klabu ya
KIMONDO inasikitishwa na taarifa hizi za upotoshwaji zinazofanywa na YANGA kwa
makusudi kabisa kuwa mchezaji wetu hana mkataba na sisi.
Kuchia suala hili likakua namna hii ni fedheha kwa klabu ya Yanga ambayo inasajili wachezaji wa kimataifa kwa mamilioni. Ni bora kuongea na KIMONDO na kumnunua mchezaji ili marumbano yaishe, nina hakika gharama yake haiwezi kufikia hata robo ya mchezaji yeyote kutoka nje ya nchi.
ReplyDelete