Filamu iliyopewa jina la AISHA imezunduliwa rasmi siku ijumaa ya tarehe 31/7/2015 wilayani Pangani chini ya shirika lisilo la kiserikali la UZIKWASA.
Aisha ni filamu ya tatu katika mfululizo wa filamu za UZIKWASA zikiangazia aina mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike. Filamu hizi ni ni sehemu mojawapo tu ya njia za mawasiliano katika kampeni shirikishi-jamii ya mabadiliko ya tabia inayofahamika kama 'BANJA BASI'!, Pangani, Tanga.

Kabla ya filamu ya Aisha iliyozinduliwa kwa kishindo hivi karibuni, shirika la UZIKWASA tayari limeshatengeneza filamu nyenigne mbili ambazo ni FIMBO YA BABA na CHUKUA PIPI, wengi wa waigizaji waliomo ni wasanii wa vijijini.
1- moja
Pia filamu hizi zinatokana na maisha halisi na utafiti wa kina katika jamii. Kwa nji hii UZIKWASA inahakikisha filamu zake zinaeleweka na zinafanya kazi kama kioo wka jamii. Lengo ni tuone, tuguswe na hatimaye tuchukue hatua ili kuleta mabadiliko.

Filamu ya AISHA inamhusu mwanamke anayeishi mjini na kuamua kurudi kijijini kwao kuhudhuria harusi ya mdogo wake. Wakati anajikumbusha maisha yake ya zamani, na kukutana na familia yake pamoja na marafiki, kunatokea mkasa wenye athari kubwa katika maisha yake.

Watu wangefumbia macho mkasa huo, lakini Aisha anaamua kupambana nao vikali ili kupata haki yake.

Filamu hii inahusu unyanyaa, aibu na wahanga kulaumiwa, na namna gani inazuia wanawake na wasichana kusema wazi. Pia inahusu baadhi ya mamlaka na viongozi kusita kufatilia ukiukaji wa haki za binadamu.

AISHA imeongozwa na mtaalamu maarufu Chande Omar, imetayarishwa kwa ushirikiano na Kijiweni Production, imefadhiliwa na A. Schindler na Swiss Development Cooperation (SDC) na kusimamiwa na shirika la UZIKWASA.

Filamu ya aisha ni kwa heshima ya wanawake wote waliopitia mikasa ya namna hii.
8- nane
Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Regina Chonjo ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, nae alipata nafasi ya kutoa hotuba yake.
6- sita
Producer wa filamu ya Aisha Bwana Emil Shivji akizungumza na wananchi waliohudhuria viwanja vya Bomani.
7- saba
Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA Dokta Vera Piroth akitoa hotuba yake ya kipeke ambayo ilikuwa katika mtindo wa hadithi pamoja na maswali, Ilipendeza sana.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...