Kamati ya maandalizi ya tamasha la ‘Kandanda Day 2015’, inatarajia kufanya tamasha lake la kila mwaka,litakalofanyika katika Viwanja vya TCC Oktoba 17
mwaka huu,Chang’ombe, Dar es Salaam.

Katika tamasha la mwaka huu,mbali na kuwepo kwa mechi kati ya Timu DizoMoja na Timu Ismail, lakini pia kutakuwa na matukio mbalimbali ya kimichezo na kijamii
yatakayoendelea.
 
Mratibu wa tamasha hilo Patrick Dumulinyi,alitanabaisha kuwa siku hiyo, kutakuwepo na mchezo wa utangulizi ambao utahusisha kituo cha kulea watoto yatima kinachojulikana kama House of Blue Hope, kilichoko Mabibo. 
“Katika tamasha la mwaka huu ambalo litabeba kauli ya Tukapige Kura, kwa makini,Tuisaidie jamii, wanakandanda wote tunapenda kuwahakikishia kutakuwepo kwa mambo mbalimbali mazuri na yataacha kumbukumbu kwa
wanasoka watakaohudhuria siku hiyo,”alisema Dumulinyi na kuongeza. 
 
“Mbali na kucheza soka,lakini tutacheza pamoja na watoto yatima pamoja na kula nao chakula cha pamoja,pia katika kuelekea siku hiyo tutakuwa tunauza T-Shirt
maalumu,ambazo tunatarajia fedha tutakazozipata tutatoa asilimia kumi ya mapato kwa ajili ya kuchangia kitu hicho, kama mwanzo wa kampeni ya tovuti ya kandanda
ya #OneBallOneTxtBook, kampeni ambayo lengo lake ni Kutoa mpira na madaftari kwa vituo na shule za msingi”

Dumulinyi,alisema kwamba kamati ya maandalizi imejipanga kikamilifu kufanya tamasha hilo kuwa bora na liwe mfano kwa makundi ya wadau wote wa soka
nchini. 
 
“Kikubwa tunachopigana nacho kwasasa ni uwezeshaji wa tamasha hilo,kwani licha ya kamati kujiandaa pamoja na kujitokeza kwa baadhi ya wadau kuunga mkono
tunachokifanya,lakini tunahitaji nguvu zaidi kutoka kwa makampuni,taasisi, mashirika na wadau binafsi,ambao tunaamini nguvu yao itasaidia kufanikisha
tamasha hilo kuwa bora zaidi,”
 
Alisema tamasha la mwaka huu ni muendelezo wa tamasha bora la mwaka jana, ambalo lilipata udhamini mbalimbali ukiwemo ule wa kampuni ya matairi nchini ya
Binslum, ambayo tayari imeshakubali kudhamini pia mwaka huu.
 
Imetolewa na Kamati ya Kandanda Day 2015
Mohamed Mkangara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...