Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kwa Chama cha Mapinduzi Bi.Samia Suluh akisalimiana na Mh;Mwigulu Nchemba ambaye ni mgombea Ubunge jimbo la Iramba hii leo,Bi.Samiah suluhu katika ziara yake ya kampeni ndani ya mkoa wa Singida,hii leo amefika Kata ya Kyengege Jimbo la Iramba kwaajili ya kunadi Ilani ya CCM ya uchaguzi ya Mwaka 2015 na kuomba kura za kishindo kwa nafasi zote za Udiwani,Ubunge na Urais ifikapo Tar.25.10.2015
Bi.Samiah Suluhu ambaye ni Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi akizungumza na Wananchi wa kata ya kyengege mambo mbalimbali anayodhamiria kuwafanyia mara baada ya kushinda hapo October 25.Kubwa amewaahidi kutatua kero ya Maji kwa Tanzania nzima ,Kujenga mabweni kwaajili ya watoto mashuleni,Kuinua Uchumi wa akina mama kupitia Mikopo mbalimbali na kupitia Utekelezaji wa Ilani ya CCM inayosema kila kijiji kimetengewa Milion 50 kwaajili ya maendeleo.Mgombea mwenza wa nafasi ya Urais Bi.Samiah Suluhu akimuombea Kura Mh;Mwigulu Nchemba kwa wananchi wa kata ya kyengege hii leo wakati wa mkutano wa kampeni za kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.Kushoto ni Mgombea Ubunge jimbo la Mkalama kupitia CCM ambaye pia alihudhuria mkutano wa Kata ya Kyenge wilaya ya Iramba.Makamu wa Rais mtarajiwa wa Kwanza Mwanamke Nchi Tanzania akimnadi Mgombea Udiwani wa kata ya Kyengege wilaya ya Iramba.Hapa akiwanadi washindi wa Ubunge Viti Maalum Mkowa wa Singida,Kushoto ni Ashyrose na Kulia ni Bi.Martha Mlata.
 Picha na Sanga Festo Jr.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kaka michuzi huna taarifa yoyote ya mkutano wa jana wa UKAWA hapo jangwani? au mtandao wako ni wa chama kimoja tu,huwezi kuwa mwana habari huru ikiwa ni blog yako ni ya chama cha mapinduzi sawa lakini ikiwa ni ya jamii sisi wadau wako ni wengi sio wote wa jamii moja.tujulishe kwa maandishi kama tuko blog siyo tutakuelewa.

    mdau.
    JANGWANI,DAR.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...