Dkt Gideon Shoo (mwenye gwanda la buluu) mwanahabari mwandamizi na mkongwe akielezea alivyoamua kuingia katika kilimo hai cha
kisasa alipotembelewa
shambani na nyumbani kwake kata
ya Kerege wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani na maofisa
kutoka Envirocare , asasi isiyokuwa ya kiserikali inayojihusisha na mazingira na haki za binadamu.
Dkt Gideon Shoo akionesha anavyozalisha mbolea ya samadi
Dkt Gideon Shoo akitembeza wageni kwenye shamba lake sehemu ya mbogamboga.
Ni jambo la
kawaida kwa mtu yeyote ajira yake inapokaribia kufikia ukomo hufikiria namna
atakavyoondesha maisha yake kwa kutafuta shughui itakayo mfanya aweze
kujiingizia kipato kwa ajili yake na famiia kwa ujumla.
Hivyo ndivyo
ilivyokuwa kwa Dkt. Gideon Shoo, mwanahabari mwandamizi na mkongwe
ambaye aliamua kuingia katika kilimo hai
cha kisasa ambacho hakitumii dawa za
kemikali kutoka viwandani .
Dakta Shoo
kwa sasa kilimo hicho anakifanya nyumbani kwenye shamba katika kata ya Kerege
wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Akizungumza
wakati alipotembelewa shambani na nyumbani kwake na maofisa kutoka Envirocare , asasi
isiyokuwa ya kiserikali inayojihusisha na mazingira , hakiza binadamu alisema
kilichomhamisha kuingia kwenye shughuli hiyo ni kutokana na kukulia kwenye
kilimo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...