Mwenyekiti wa Mtandao wa Kimataifa wa Wabunge  (PGA) Mhe.  Pindi Chana ( MB) akimkabidhi Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa,  Bw.Mogens Lykketoft,Tamko la  wabunge lenye sahihi 607 za wabunge kutoka mataifa 70 la  kutokomeza ndo za utotoni na za kulazimisha katika hafla fupi iliyofanyika  Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu.
 Mwakilishi wa Kudumu wa Zambia katika  Umoja wa Mataifa, Balozi Dr. Mwaba Kasese-Bota akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo alianisha mipango mbalimbali inayofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wa kimila katika kuzunguia ndoa za utotoni na za kulazimishwa.

Na  Mwandishi Maalum, New  York
Mtandao wa Kimataifa  wa Wabunge kutoka  Mabunge mbalimbali  Duniani (PGA),  umemkabidhi Rais wa Baraza Kuu la  70 la Umoja wa Mataifa Bw. Mogens Lykketoft,  tamko   la kukomesha ndoa za utotoni  na za kulazimishwa kwa watoto wa kike.

Akikabidhi tamko hilo lenye sahini  Zaidi ya 607   kutoka nchi 70 Mwenyekiti  wa Mtandao huo wa wabunge,  Mhe. Pindi Chana na ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,  Jinsia na  Watoto amesema, kukabidhiwa kwa tamko  hilo kwa  Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  kunakwenda sambamba na  maadhimisho  ya siku ya mtoto wa kike ambayo   huadhamishwa  kila  Octoba ya mwaka.

Mwenyekiti wa  PGA, amesema wakati wa  hafla hiyo fupi iliyofanyika hapa  Umoja wa Mataifa, siku ya Jumatatu kwamba,  ushirikiano wa wadau mbalimbali hasa  wabunge , serikali na asasi za kiraia ni  muhimu sana ikiwa jumuiya ya kimataifa  inataka kuondokana na kumaliza tatizo la ndoa za utotoni na za kulazimishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera sana na pongezi za dhati Bi Ellen Maduhu kutuwakilisha, pia pongezi za dhati kwa washiriki wote. Ni kweli kabisa imefikia wakati sasa lazima kuwepo na mikakati thabiti na sheria imara za kumlinda, kumtetea na kumsaidia kwa kila hali mtoto wa kike na kulitokomezea mbali suala zima la ndioa za utotoni na hata za kulazimishwa pasina ridhaa yake, kwani vitendo hivyo vimekuwa vikimnyima fursa na nafasi mbali mbali katika kujiendeleza kielimu, kimaendeleo na katika fani nyingine mbali mbali ambazo zingeweza kumkombowa katika maisha yake ya baadae na badala yake kujikuta yupo katika ndoa asizozitarajia katika umri mdogo kabisa na pengine kwa kulazimishwa bila kutaka au kukubali kwa ridhaa yake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...