Naibu Mkurugenzi mkuu wa benki M Bi Jacqueline Woiso akitoa ripoti ya fedha ya benki hiyo katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka huu wa 2015 mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hoteli ya Hyatt Regency hii leo. kushoto kwake ni mkurugenzi wa mawasiliano wa benki hiyo bw. Allan Msalilwa

BENKI M leo hii imetangaza ripoti yake ya fedha katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka huu wa 2015, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency leo hii.

Akizungumza katika mkutano huo, Naibu mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Bi. Jacqueline Woiso alisema kuwa kwa upande wa rasilimali, mizania ya benki imeendelea kukua kwa asilimia 19% kufikia bilioni 823.43 bilioni katika robo ya tatu ya mwaka 2015, kutoka sh 689 bilioni za mwezi December 2014. Hiki ndio kipimo cha ukubwa wa benki au taasisi yoyote  ya kifedha ( Balance sheet size).

Bi Woiso aliendelea kusema kuwa “amana za wateja pia zimeongezeka kufikia 696.22 Bilioni, ni ongezeko la asilimia 19% kutoka December 2014. Hii inadhihirisha imani kubwa iliyojengwa na jamii kwa ujumla”.

Pia mikopo katika sekta za uchumi, sehemu kubwa ya mikopo iliyotolewa na benki hiyo kipindi cha robo mwaka huu ni katika sekta ya Kilimo, uzalishaji viwandani, biashara, Utalii pamoja na sekta ya Ujenzi na makazi. Pamoja na ongezeko hilo benki hiyo imeendelea kuwa na asilimia ndogo sana ya mikopo isiyozalisha faida ambayo ni asilimia 2.6% ya jumla ya mikopo yao.

Faida kabla ya kodi (Profit Before Taxes) imeongezeka kwa asilimia  32% kufikia sh 17.34 bilioni kutoka sh 13.12 bilioni September mwaka 2014. Ongezeko hili limechangiwa zaidi na ongezeko lilitokana na mapato yasiyotokana na riba. Faida katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka jana ilikiuwa ni sh.15.09 bilioni na hivi sasa ni sh.16.25 Bilioni.

 Mafanikio yetu yanatokana na ufanisi mkubwa katika teknologia tunayotumia katika kufanya miamala mbali mbali pamoja na bidhaa na huduma zenye ubora wa hali ya juu katika soko la kibenki nchini”. alisema Bi Woiso.

Aliongeza kuwa katika kipi hicho cha robo ya tatu ya mwaka 2015, zipo changamoto kubwa zilizojitokeza kama vile uhaba wa fedha katika soko la ndani la kifedha (domestic market) na kusababisha viwango vya riba kuongezeka kwa takriban asilimia 5.

“Vile thamani ya shilingi iliendelea kuporomoka kutoka viwango vya dola 1/sh 2,000 hadi kufikia dola 1/sh.2,200. Athari za kushuka thamani ya sarafu yetu ni kubwa hususan kwa nchi kama Tanzania ambayo uchumi wetu unategemea bidhaa za nje kwa kiwango kikubwa sana, pia gharama za maisha zinaongezeka kwa jamii kwa ujumla”, alimalizia Bi. Woiso.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...