Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Michael Mhando akikagua Kituo cha Kisasa cha Matibabu kilichopo katika Hospitali ya Mkoa Dodoma. Kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akionesha ufunguo wa kituo hicho baada ya kukabidhiwa na baadae alikikabidhi rasmi katika uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Na Mwandishi Wetu

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhiwa kituo chake cha matibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika.

Makadhiano hayo yalifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Uongozi wa NHIF, hospitali ya mkoa na timu ya wakandarasi akiwemo mshauri mkuu wa mradi huo wa kampuni ya Nosuto Associates.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando amesema kukamilika kwa jengo hilo ni hatua kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na kazi iliyoko sasa ni ya ununuzi wa vifaa na samani za jengo ili lianze kutoa huduma kabla ya sikukuu ya Krismasi.

Amesema timu ya wataalamu kutoka Sekteratarieti ya mkoa tayari iko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua vifaa tiba mbalimbali vitakavyotumika. Ameongeza kuwa vifaa vyote hivyo pamoja na samani za jengo hili vitalipiwa na Mfuko wa NHIF.

Kituo hicho cha matibabu cha kisasa kinayo mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika utoaji wake wa huduma ikiwemo miito kwa wauguzi, utayarishaji wa madai na utambuzi wa wagonjwa.

Amesema malengo makuu ya ujenzi wa kituo hicho ni kuwa na kituo cha kisasa kitakachowezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na umma wa watanzania kwa ujumla kupata huduma bora za matibabu wanapokuwa Dodoma katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.

Naye Mkurugenzi wa fedha, Mipango na Uwekezaji wa NHIF Bw. Desudedit Rutazaa amesema Kituo hicho vilevile kitasaidia kuwepo na watalamu wenye uzoefu nchini kwani itakuwa ni sehemu ya kujifunzia kwa wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari na utabibu wawapo masomoni katika mkoa wa Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania. Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma_sehemu ya mapokezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...