Na Shamimu Nyaki-Maelezo 

Serikali imewaagiza watumishi wa umma kushiriki zoezi la usafi wa  nchi  litakalofanyika tarehe 9 disemba mwaka huu katika maeneo yao wanaoishi.

Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw Assah Mwambene alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijin Dar es salaam na kusema kwamba Watumishi wa Umma  wanatakiwa wabaki nyumbani na kufanya usafi katika maeneo yao na  yale watakayo pangiwa na viongozi wa mitaa wanayoishi.

“Kila mwananchi ahakikishe eneo lake ni safi”Alisema Mwambene.

Mkurugenzi ameongeza kuwa Watumishi wa Umma hawataenda kazini badala yake  watabaki  nyumbani na kufanya usafi kwa kushirikiana na wananchi kusafisha maeneo yanayozunguka mitaa wanayoishi ikiwemo hospitali,kuzibua mitaro iliyoziba pamoja na kuzoa taka zilizolundikana sehemu ambazo sio rasmi.

Ameongeza kuwa muongozo kuhusu namna zoezi la usafi litakavyotekelezwa umeshatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI  kwa Uongozi wa Mikoa hadi Mitaa na kilichobaki ni utekelezaji tuu wa agizo hilo kwa kila mwananchi sehemu anayoishi,anayofanyia shughuli nyingine za kila siku kuhakikisha anafanya usafi.

Aidha Mkurugenzi amewataka viongozi wa kila eneo kutengeneza utaratibu mzuri ambao utafanikisha zoezi la usafi  kufanikiwa kwa kuhakikisha wanasimamia kwa ukamilifu na kuwahimiza wananchi kuwa na tabia ya kusafisha maeneo wanaoishi kwa kuwa ni wajibu wao kufanya hivyo.

Hata hivyo tarehe tisa disemba kila mwaka huwa ni siku ya kusherehekea Uhuru wa Tanganyika uliopatikana miaka hamsini na nne iliyopita lakini kwa mwaka huu itaadhimishwa kwa kufanya usafi nchi nzima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tunaomba msambaze magari ya kuzolea taka ili uchafu unaotolewa kwenye mifereji uwekwe kwenye magari maalum. Mtindo wa kuweka taka pembeni mwa mitaro huwa si mzuri. Kwani baada ya muda taka hurudishwa tena kwenye mitaro. Mapipa ya kutupia uchafu yasambazwe Dar es Salaam nzima. Mnataka watu watupe wapi uchafu. Huu uwe mpango kapambe wa kudumu. Tunahitaji vitendea kazi kama hivyo. Dar safi inawezekana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...