Na Bashir
Yakub
Hatua unazopitia unapohitaji
hatimiliki ni tofauti
na hatua unazopitia
unapohitaji kubadilisha jina
katika hatimiliki( transfer).
Kutafuta hati na
kubadilisha hati ni michakato miwili
tofauti. Makala kadhaa
zilizowahi kuandaliwa
zilieleza namna ya
kubadilsha hati na
sio namna ya kutafuta
hati mpya. Makala ya
leo yanaeleza namna
ya kupata hati
mpya.
1.TOFAUTI YA
KUTAFUTA HATI NA KUBADILISHA
HATI.
Unapotafuta hati maana
yake ni kuwa
ardhi yako haikuwa
na hati kabisa
na sasa unaanza mwanzo
kabisa kutafuta. Kwa wamiliki
wa ardhi za
namna hii mara
nyingi ni zile
ardhi zenye mikataba
ya kununulia( sale
agreement),ardhi zenye barua ya
toleo( letter of offer), na
nyingine zinakuwa hazina
waraka wowote. Kwa ardhi
za namna hii unaposema
unahitaji hati ni
lazima uanze mwanzo
kabisa.
Aidha kubadilisha hati
maana yake ni kuwa,
hati inakuwepo isipokuwa
inabadilishwa kutoka jina
moja kwenda jingine.
Pengine ni muamala
wa mauziano kwahiyo
jina linatoka kwa
muuzaji kwenda kwa
mnunuzi au linatoka
kwa marehemu kwenda
kwa msimamizi wa
mirathi. Kwahiyo kubadilisha ni
kubadilisha tu na
wala sio kutafuta
hati mpya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...