JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA.

MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU KATIKA SHULE YA MSINGI NZOVWE ILIYOPO JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ERICKA MWASIKILI [08] MKAZI WA NZOVWE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 239 CCU AINA YA MITSUBISHI FUSO IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE GEORGE LWINGWA [40] MKAZI WA ISANGA JIJINI MBEYA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 10.02.2016 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO ENEO LA NJIAPANDA ITENDE, KATA NA TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA. UPELELEZI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO HASA KWA KUWEKA UANGALIZI PINDI WANAPOTUMIA BARABARA.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...