Watu kadhaa wamenusirika kifo huku wengine zaidi ya sita wakijeruhiwa vibaya baada ya kontena kuagukia magari katika eneo la Tabata reline jijini Dar es salaam. https://youtu.be/XeX8GC62j3M 

Hospitali ya taifa ya Muhimbili inakusudia kuanza huduma za usafishaji na upandikizaji wa figo ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya hospitali hiyo kuipunguzia serikali mzigo wa kusafirisha wagonjwa nje yanchi. https://youtu.be/WrI6eEXE5h4   

Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita onyo kali kwa walimu wakuu mkoani humo huku akiwataka walimu waliopokea michango kutoka kwa wanafunzi kurudisha fedha hizo mara moja.https://youtu.be/ftkL6pvNti4  

CH10:Rais John Magufuli atembelea wodi ya wazazi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na kujionea adha wanayokumbana nayo wazazi huku akiahidi kutatua changamoto zinazowakabili.http://simu.tv/uELVbnp https://youtu.be/x1N9NvSuxzg  

Katika hali ya kusikitisha wafanyabiashara wanaopanga bidhaa barabarani katika maeneo ya kariakoo wadaiwa kumpiga kijana mmoja na kumuua baada ya kudaiwa kukanyaga bidhaa zinazopangwa chini. https://youtu.be/aEvoCeWJT68  

Jeshi la polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu 20 kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mifugo wilayani Mvomero.https://youtu.be/_L_m0i9XQro  

Meneja wa fedha  wa shirika la ndege Tanzania ATCL, Steven Kasubi asimamishwa kazi kwa tuhuma ya ubadhilifu wa fedha za umma;https://youtu.be/cEzy0q8POzI  

Baadhi ya wananchi katika Kitongoji cha Mkanyageni A kilichopo kata ya Ruvu wilayani Same mkoani Kilimanjaro waishangaa serikali ya kijiji  kwa kuuza eneo wanalotumia kwa ajili ya shughuli za kilimo;https://youtu.be/MZe2MZEy2Ws  

Inaripotiwa kuwa zaidi ya nyumba 100 katika kata ya Ilemela mkoani Mwanza zabainika kuunganishiwa umeme kinyemelahttps://youtu.be/KTQiyd_I_pM  

Mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya kaskazini kwa kushirikiana na jeshi la polisi imefanikiwa kukamata shehena ya vipodozi vinavyotengezwa kinyume na sheria;https://youtu.be/DaXoDWSv7uE  

Serikali ya waagiza watendaji wa mpango wa urasimishaji wa rasilimali za wanyonge kushirikiana na taasisi za kibiashara ili kuharakisha zoezi la urasimishaji wa biashara nchini;https://youtu.be/YY0fA0CvsbE

Taasisi za kifedha nchini zaombwa kupeleka huduma za kibenki katika maeneo ya vijijini; https://youtu.be/UWaQZAsmlNw  

Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam yabadili safari yake ya kuelekea nchini Mauritius mpaka siku ya Ijumaa; https://youtu.be/-LMIAptlomg  

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya  wanawake Twiga Stars, Nasra Mohammed awataka watanzania waisaidie timu hiyo ili ifanye vizuri katika michezo yake kufuzu kuelekea fainali za mataifa ya Afrika kwa wanawake; https://youtu.be/UKjmfv6ov7c  
  
Wafanyakazi wa wizara ya Uwezeshaji  Ustawi wa jamii , Vijana , Wanawake na Watoto visiwani Pemba watakiwa kutimiza wajibu wao; https://youtu.be/WdDgMnv8cP0  

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein ahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 30 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa mahakama ya watoto; https://youtu.be/HxsadIPRIAs

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wachunguzwe Mawakala wote hata wanaoiuzia Serikali tiketi. Wote mtandao tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...