Na Vivi Machange
Ukitaka kufanikiwa katika jambo lolote ni muhimu kuwa na mipango iliyoandaliwa. Vilevile katika mapambo ya nyumba mipango ni jambo muhimu. Kama toka awali uliweka mipango ya namna utakavyopamba nyumba yako hii ninayoongelea hapa itakusaidia. Laa haukuweka mpango bado hujachelewa, unaweza kuanza leo. 
Mpango ninaozungumzia hapa ni wa rangi ya kuta na sakafu za nyumba toka awali. Ni kwamba kama ukiwa na kuta na sakafu zenye rangi ambazo haziegemei upande wowote, unaweza kubadili muonekano wa chumba chochote kirahisi sana kwa kubadili tu vitupio vya mapambo. Rangi zisizoegemea upande wowote sio lazima tu ziwe jamii ya nyeupe au krimu bali ni rangi zote nyepesi na zilizotulia ambazo ni pamoja na kijivu na bluu bahari. 
 Kama unataka chumba kiwe sehemu ya kupumzikia unatakiwa utumie rangi zilizopoa. Rangi zilizopoa ambazo ni bluu, kijani na zambarau maana yake ni kwamba zikiwa mahali zinaleta hisia ya utulivu. 
Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...