Ikiwa bado Singapore inaendelea na mkakati wake wa kua “Smart Nation” imeanisha kuweza kufikia hapo lazima swala la usalama mitandao liwe muhimu zaidi “Top priority”. 
Hii ni kutokana na uhalisia kua Nchi inapokua ya kisasa zaidi na kutumia kwa wingi mifumo yaki Teknohama katika maeneo mbali mbali uhalifu mtandao nao unaongezeka.

Mwaka jana (2015) katika kuliendea hili la kuhakiki Usalama mtandao unashika nafasi ya juu kwa taifa hilo linalokua kwa kasi barani Asia, walianzisha wakala wa usalama mtandao “Cybersecurity Agency” ambapo uliiunganisha vitengo vyote vidogo vya usalama mitandao na kukuza ushirikiano na sekta binafsi nchini humo.
Hatua hiyo ilipongezwa na wana usalama mitandao Duniani kote na binafsi kuliandikia katika andiko linalosomeka “KWA KUBOFYA HAPA”. 
Tayari nchi hiyo pia ina mpango wa kimkakati wa miaka mitano wa kitaifa wa usalama mtandao “National Cybersecurity Master plan” ambapo inategemewa kuwekeza zaidi katika kulinda miundo mbinu yake ya TEHAMA pamoja na taarifa zake pamoja na Wananchi wake. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...