Na Sultani Kipingo
Katika kunogesha Libeneke hili, Globu ya Jamii kuanzia leo linazindua makala mpya maalumu itakayojulikana kama “MULIKA VIJIPU UPELE”,  lengo kuu likiwa ni kuanika mambo ya  uzembe, kutowajibika, kujisahau, huduma mbovu, kufanya kazi kwa mazoea na madudu mengine mengi yanayokera jamii. Hii ni katika kutoa mchango wetu mdogo katika kuisaidia serikali ya awamu ya tano kuweka mambo sawa.

Makala hii itakujia wakati wowote “Vijipu Upele” vitapoonekana popote pale nchini. Na katika kutekeleza na kufanikisha hili, pia tunakaribisha michango ya picha na habari kutoka kwenu waheshimiwa wadau wetu. Tuma kwa kupitia email address ya issamichuzi@gmail.com au kwa WhatsApp namba +255 754 271 266, nasi tutairusha hewani mara moja. Hakikisha unataja nini, wapi na lini.

Kwa kuanzia na kama mfano wa zoezi hili, mmulika “Vijipu Upele” wetu ametembelea mji wa Dodoma na kuvinjari katika bustani maarufu  ya  Nyerere Square, na kukuta wana Dodoma wengi wako pale wakipunga upepo ama utengeneza kucha zao na urembo mwingine ama kupiga picha kama ilivyo ada ya mahali hapo.

Lakini  lahaula! Hali aliyoikuta mmulikaji "Vijipu Upele" wetu kwenye mnara wenyewe wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni ya kusikitisha.... 

Wanasema bandubandu humaliza gogo. Na endapo hakuna juhudi za makusudi za kuuokoa mnara huo hazitafanyika haraka, basi mambo yatakuwa mengine, maana  karibu sakafu ya mnarani hapo sio tu inameguka na kuvunjika, bali pia karibu slabs za sakafu yote zimelegea. Hatuna uhakika kwamba tatizo ni kutumika sana kwa watu kutembelea kila siku kwa wingi, ama mafundi waliofanya kazi hiyo alilipua kazi. 
Jionee mwenyewe taswira hizi.....





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. nani ni msimamizi wa eneo hili? Manispaa au CDA?

    ReplyDelete
  2. Hivi hapa ni wapi wadau!

    ReplyDelete
  3. Hii safi sana. Itatusaidia kuwajibika katika ngazi ya vijipu vidogo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...