Baada ya jana kuiripoti habari ya lile dampo haramu la temeke mwisho, sasa kijipu upele kilichokuwa kikisumbua na kukera watu wa Temeke Mwisho, Kimetumbuka kabla hata ya kupakwa kitunguu swaumu. Lile dampo korofi limesafishwa usiku mzima wa kuamkia leo, na hali sasa ni kama unavyoiona katika picha.

Somo hapa ni kwamba;

1. Tusifanye kazi kwa mazoea, mpaka watu walalamike baada ya kudhurika- reactive mode 
 2. Kama uwezo wa kusafisha uchafu ule kwa usiku mmoja upo, kwa nini msingefanya hayo tangia siku za nyuma

SISI WAKAZI WA KARIBU NA ENEO HILI, TUNAOMBA DAMPO HILI LIONDOLEWE HAPA, NA KIWANJA HIKI CHA WAZI KILICHOVAMIWA WARUDISHIWE VIJANA WETU WA TEMEKE WAENDELEE KUKITUMIA KWA MATUMIZI CHANYA.
Najua wahusika mnaisoma Globu hii ya Jamii na suala hili linaloharibu mandhari nzuri ya temeke mwisho mtalifanyia kazi.
Malori yakipishana kuondoa uchafu uliokuwa umerundikwa kwenye dampo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. I can only say one word here:impressive

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...