Kaimu Katibu Mkuu uvccm Taifa SHAKA HAMDU SHAKA akikabidhi kadi kwa wanachama wapya wilaya ya Mwanga

Kaimu katibu mkuu UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akifungua shina la wakereketwa wa CCM katika kijiji cha Mtalang'a
kikundi cha ngoma kutoka katika kabila la kichaga kikitumbuiza wakati wa kaimu katibu mkuu wa UVCCM akiwasili wilayani Mwanga 
 
Na Woinde Shizza, Mwanga

Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umewataka wananchi wa mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania kukataa na kuzikwepa siasa za uzawa na ukanda kwasababu ubaguzi ni dhambi isiyosamehewa na mungu.

Wametakiwa kutambua kuwa ubaguzi ni zaidi ya laana ambayo ikiemea na kujengeka katika jamii kuiondosha kwake ni kazi ngumu na kwamba kafara yake lazima maisha ya watu yapotee au damu imwagike.

Hayo yameelezwa leo na Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu shaka wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika kijiji cha Mtalang'a kata ya Mwanga mkoani hapa.

Shaka alisema ni aibu binadamu aliyestaarabika, kupata elimu akawa anaishi, kupigania madaraka., vyeo au utawala kwa kutumia maneno au sera za ubaguzi wa dini, ukabila, uzawa au ukanda.

Aidha aliongeza kuwa baada ya miaka 52 ya uhuru na Muungamo wa mataifa ya Tanganyika na zanzibar, anapotokea kiongozi au chama cha siasa kinachofanya shughuli za kisiasa kwa kueneza sumu ya uzawa na watu kupiga kura kwa ukanda ni hatari mpya mbele ya watanzania.

"Ndugu zangu wananchi wa mikoa ya Kaskazini kuna hatari inawanyemelea, msipoitahadhari na kukwepa, ikiwaingia kutoka kwake ni mbinde, ili ifanyike kafara ya kuondoa laana hiyo si ajabu damu ikanwagika "alisema Shaka.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2016

    UVCCM sasa wananchi kuchagua chama cha siasa cha kitaifa kilichosajiliwa rasmi na msajili wa vyama vya siasa nchini na ikatokea chama kilichochaguliwa na wananchi siyo CCM ni sawa na siasa za ukanda na uzawa ? mlitaka CCM ishinde kwa zaidi ya kishino yaani iwe asilimia 100 nchi nzima ?!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...