TIMU ya Uchukuzi SC iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, imeibuka kinara kwenye mashindano ya Mei Mosi baada ya kutwaa vikombe 11 vya michezo mbalimbali.
Timu hiyo imetwaa ubingwa katika michezo ya netiboli, baiskeli na bao (wanaume), kamba (wanawake na wanaume); huku vikombe vya ushindi wa pili ni vya michezo ya bao (wanawake) na draft (wanaume); wakati vya ushindi wa ni katika soka, karata (wanaume), riadha (wanawake na wanaume).
Hatahivyo, kutokana na uwingi wa vikombe timu hiyo inatarajia kutangazwa mshindi wa jumla kesho kwenye sherehe za Mei Mosi na kukabidhiwa kombe na Mh. Rais John Magufuli.Timu nyingine na idadi ya vikombe zilizopata ni Tamisemi saba kikiwemo cha ubingwa wa soka baada ya kuwafunga GGM katika fainali kwa magoli 2-0, huku TPDC wakiwa na vikombe vitano sawa na Tanesco.
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wamejikusanyia vikombe vinne, Ujenzi vikombe viwili, na Mawasiliano, Ukaguzi na Halmashauri ya Nyasa kila mmoja wana kikombe kimoja kila mmoja.Awali katika michezo iliyochezwa jana timu ya Uchukuzi SC iliwafunga Tamisemi kwa magoli 18-15 katika mchezo wa netiboli, ambapo wafungaji wake Tatu Kitula na Matalena Mhagama waliwapeleka puta wapinzani wao na hadi mapumziko walikuwa mbele kwa magoli 11-7.

Washindi wote walikabidhiwa kombe na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), Mussa Kalala, ambaye katika hotuba yake aliwashutumu viongozi walioshindwa kupeleka timu zao kwenye mashindano hayo na kusema michezo mahala pa kazi husaidia kuijenga miili ya wafanyakazi kuendelea kuwa mikakamavu na kuwa na afya bora, ambapo hutoa huduma bora iliyotukuka na kuzalisha tija zaidi.
Naye Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya Mei Mosi, Joyce Benjamin alisema wamesikitishwa na ushiriki wa timu chache mwaka huu, ambazo ni 11 pekee ukilinganisha na mwaka jana zilikuwa 28.
“Pamoja na kamati yetu kusikitika kwa uchache wa timu zilizoshiriki katika michezo ya mwaka huu, hata mkuu wa mkoa katika hotuba yake ya uzinduzi wa michezo hii naye alisikitika ambapo wote kwa pamoja tumesikitishwa sana na viongozi wengi kutoleta timu zao hatujii kwa sababu ya kumuogopa Mh. Rais pengine kwanza labda amekataza michezo, au wana sababu zingine tu zao binafsi,” alisema Benjamin.
Mwanaisha Athuman wa Uchukuzi SC akipokea kombe la ubingwa wa netiboli kutoka kwa mgeni rasmi Mwenyekiti TRAWU, Mussa Kalala, katika mashindano ya Mei Mosi.Wachezaji wa Uchukuzi SC wakiwa wamevipanga vikombe 11 walivyotwaa kwenye michezo mbalimbali ya Mei Mosi, iliyomalizika juzi mkoani Dodoma.Bingwa wa baiskeli Chaptele Muhumba wa Uchukuzi SC akiwa amekumbatia kombe alilotwaa kwenye mashindano ya Mei Mosi.Wachezaji na viongozi wa Uchukuzi SC wakishangilia baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya Mei Mosi yaliyomalizika juzi mkoani Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...