Na Lorietha Laurence

Vijana wamehimizwa kuendeleza upendo na uzalendo katika kutambulisha Taifa la Tanzania ikiwemo kutangaza utamaduni wake kwa mataifa mengine  Barani Afrika na Duniani kwa ujumla. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utamaduni wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi, Lilian Beleko jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za kuzindua klabu za Vijana ya Mwalimu Nyerere chini ya usimamizi wa Taasisi ya Ariseamka Afrika ikiwa na lengo la kuwapatia vijana elimu ya msingi kuhusu historia ya ukombozi wa bara la Afrika na masuala mbalimbali ya kijamii.
“Klabu ni jambo jema na zuri kwa vijana wa sasa ukizingatia wengi wao hawakuwepo wakati ukombozi wa bara la Afrika hivyo kupitia klabu hizi mtajifunza mengi” alisema Bi.Beleko.
Aidha aliongeza kuwa viongozi wa Afrika walijitolea kwa moyo mmoja kuonyesha uzalendo kwa kuwaunganisha waafrika katika kupigania uhuru wa bara la hilo ili kuwakomboa kutoka mikononi mwa wakoloni na kuweza kujitegemee kwa kuwa na viongozi wake.
Naye Mwanzilishi wa Taasisi ya Ariseamka Afrika Bi Kulthum Maabad ameleza kuwa ili vijana waweze kujikomboa kutoka katika umaskini ni muhimu kwanza kujikomboa kifikra kwa kupata elimu muhimu ikiwemo ya uzalendo wa kuitumikia nchi zao kwa uaminifu.
Kwa upande wake Msaidizi Maalum wa mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere nchini ameeleza kuwa kuna umuhimu wa kujifunza na kuujua mchango mkubwa uliofanywa na Mwalimu Nyerere katika ukombozi wa bara la Afrika kwa kusoma vitabu vyake na kupitia nukuu zake
Uzinduzi wa klabu za Vijana ya Mwalimu Nyerere umeenda sanjari na kilele cha maadhimisho ya wiki ya ukombozi wa afrika ambapo hukumbukwa kwa kuwaenzi waasisi wa upigania uhuru kwa kuwepo kwa maonyesho mbalimbali ya Sanaa,Lugha na Utamaduni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Matumizi yasiyo sahihi katika hotuba hiyo inaonyesha wazi hawa wapiga debe wa uzalendo kupitia utamaduni hawajui wala kuelewa utamaduni ni nini na unawezaje kueleweshwa kwa watu. Lugha na sanaa ni vipengele muhimu vya utamaduni, hivi si vitu au masuala ya kutamkwa pamoja na utamaduni kama vile ni vitu tifauti. Huyo Beleko na Maabadi nahisi ni wababaishaji nawashauri warejee chapucho la Wizara ya Utamaduni wa Taifa na Michezo la 1979 lililoitwa: UTAMADUNI CHOMBO CHA MAENDELEO. Humo watajifunza mengi bila shaka wamefika hapo kupotosha watu kiasi hiki bila kujijua, kazi yao ni kubwa ila hawaifanyi kwakuwa hawaijui!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...