Dar es salaam, Wanawake wakulima wadogowadogo wakiongozwa na waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloratibiwa na shirika la Oxfam, wamekutana pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali na baadhi ya wanafunzi kutoka elimu ya juu, Tanzania kujadili Bajeti ya Kilimo kwa mwaka 2016/17 na changamoto za mabadiliko ya Tabia Nchi.

Akifungua Mkutano huo wa siku tatu, Meneja utetezi wa Oxfam Tanzania, Bi. Eluka Kibona alisema kuwa lengo la kuwakutanisha wakulima hao na wadau ni kufanya majadiliano juu ya Bajeti ya kilimo na Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa kuwa hali ilivyo sasa ni kwamba wakulima wengi hasa wadogowadogo hawapati nafasi ya kushirikishwa katika masuala ya bajeti hiyo, hivyo mkutano huo utasaidia kuibua changamoto mbalimbali ambazo zitatakiwa kutatuliwa bila kusahau suala la mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yataathiri kwa kiwango kikubwa katika kilimo.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa Programu Forum CC, Bi. Rebecca Muna alisema mabadiliko ya Tabia Nchi yamekuwa yanaendelea kuathiri zaidi wakulima wadogo wadogo hasa waliopo vijijini, hivyo kupitia mkutano huo wakulima wanapata elimu ili kukabiliana na mabadiliko hayo.

Akieleza kwa undani juu ya Mabadiliko ya tabia nchi mwezeshaji kutoka Forum CC, Faizal Ally alisema kwamba changamoto kubwa zaidi ya mabadiliko ya Tabia nchi ni pamoja na maji chumvi kuingia nchi kavu na kuathiri ukuaji wa mazao, kuongezeka kwa joto, misimu ya mvua zisizotabirika, kupungua kwa kina cha maji katika mito na maziwa, kuongezeka kwa majanga ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na mafuriko, ukame na vimbunga na kuongezeka kwa magonjwa ya mazao.

Alisema kuwa mambo yote hayo yamekuwa yakichochea wakulima na wafugaji kukosa maeneo ya malisho kwa ajili ya mifugo na kuongeza kuwa ili wakulima waweze kukabiliana na changamoto hiyo ya mabadiliko ya Tabia nchi wanatakiwa kujifunza mbinu mbalimbali ikiwemo kuvuna maji ya mvua, kutumia umwagiliaji wa matone, matumizi ya mbegu bora zinazostahimili magonjwa na Ukame, kilimo mchanganyiko/mseto, matumizi ya mbolea asili na kuongeza thamani ya mazao.

Nao wakulima hao kwa nyakati tofautitofauti walizungumzia suala zima la bajeti ambapo walisema kuwa changamoto nyingi wanazozipata kwa kutoshirikishwa kwenye bajeti kuu juu ya kilimo zinasababisha wasifikiwe na elimu na huduma mbalimbali zitakazowasaidia kwenye shughuli zao za kilimo hivyo basi kupitia mkutano huo wameomba kusikilizwa maoni yao hasa wakati wa uandaaji wa bajeti kwa ujumla kwa kuwa wao ndiyo walengwa namba moja kwenye sekta ya kilimo nchini.

Meneja utetezi kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Tanzania Bi. Eluka Kibona akifungua mafunzo juu ya uelewa wa Bajeti ya Kilimo na Mabadiliko ya Tabianchi yanavyoathiri sekta ya kilimo Tanzania hasa wakulima wadogo wadogo.
Mkurugenzi wa Forum CC Bi. Rebecca Muna akielezea umuhimu wa mafunzo hayo yatakavyoweza kuwasaidia wakulima wadodogo katika kukabiliana na tatizo la Mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa katika kikundi kujadiliana maswala mbalimbali juu ya namna ya kuandaa bajeti.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mafunzo hayo wakiwa wanatazama mfano wa jarida linalo onesha jinsi bajeti inavyo andaliwa.

Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Picha na Fredy Njeje .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...