Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongozwa na wafanyakazi wa Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma kukagua baadhi ya majengo wanayoishi wazee hao ili kuona namna ya kuyaboresha kadiri inavyowezekana wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akitoa Zawadi ya Sabuni kwa viongozi wa wazee wa Makazi ya Kibirizi Katibu Makazi hayo Bi. Veronica Nyaga na Mwenyekiti Bw.Hamisi Sabuni. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...