Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameendelea na utaratibu aliojiwekea wa kusikiliza Kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi kila siku ya Alhamisi ya mwanzo wa mwezi na siku ya alhamis ya mwisho wa mwezi, kama kawaida siku ya leo mamia ya wananchi wamejitokeza Mbele ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha kero zao.

Mkuu wa Mkoa amewataka wakuu wa wilaya na watendaji wa ngazi zote kuwasikiliza wananchi na kutatua Kero zao "Kero Nyingi hapa ni za Halmashauri, Wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wakuu wa Idara tafadhalini hakuna jambo kubwa katika Uongozi kama kuwa Karibu na unaowaongoza, kuwa msikivu na kushughulikia matatizo yao kwa umati huu ni dhahiri hamjatimiza majukumu yenu na kwa kuwa MaDc, ma Ded  ni wapya sasa anzeni kazi hii kwa kasi "

Amelitaka jeshi la Polisi kuharakisha upelelezi wa kesi na pia kuepuka vitendo vinavyolalamikiwa kwa baadhi ya Askari kubambikizia Wananchi kesi
Amehaidi kuendeleza utaratibu huu kwa muda wote mpaka siku atakapofika ukumbini akute hakuna Mwananchi aliyeleta Kero.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akiendelea kuratibu na Kuandika baadhi ya kero Sanjari na Afisa Tawala wa Mkoa wa Mbeya Mh.Mariam Mtunguja katika ukumbi Mdogo uliopo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Jijini Mbeya.
Kutoka Shoto ni Mkuu wa Wilaya Ya Mbeya Mjini mh,William Mtimika, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla na Afisa Tawala wa Mkoa wa Mbeya Mh.Mariam Mtunguja Wakiendelea na kazi ya kunukuu kero za wananchi walio hudhuria kuwasilisha kero zao (Hawapo Pichani).

Baadhi ya Wananchi wa wakitoa Kero Zao mbele ya Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya Mh.Amos Makalla.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...